Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 557
- 1,039
Mwezi Novemba, 2025 Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imefanya operesheni mbalimbali zilizofanikisha ukamataji wa jumla ya kilogramu 3,799.22 za dawa za kulevya, kuteketeza ekari 18 za mashamba ya bangi pamoja na kutaifisha mali za wahalifu wa dawa za kulevya zenye thamani ya shilingi Bilioni tatu na milioni mia tatu na nne (3,304,000,000/=). Watuhumiwa 84 walikamatwa kuhusiana na dawa hizo.
Katika kuendeleza hatua za kukabiliana na uhalifu wa dawa za kulevya, Mahakama kuu divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ilitoa maamuzi ya kutaifishwa kwa mali zenye thamani ya Tsh. Bilioni Tatu na milioni mia tatu na nne (3,304,000,000/=) za watuhumiwa Saleh Khamis Basleman na Gawar Bachi Fakir ambao wanatuhumiwa kwa makosa ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya. Mali hizo zinajumuisha nyumba, viwanja na magari.
Maombi ya kutaifishwa kwa mali hizo yaliwasilishwa mahakamani hapo kufuatia uchunguzi uliofanyika na ikabainika kwamba, watuhumiwa hao wanamiliki mali ambazo zilipatikana kwa njia za uhalifu wa biashara ya dawa za kulevya. Utaifishaji wa mali hizo umefanyika chini ya Sheria ya Mazao ya Uhalifu Sura ya 256 ikisomwa pamoja na Sheria ya Uhujumu Uchumi na Uhalifu wa Kupangwa Sura ya 200 na Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Namba 5 ya mwaka 2015.
Utaifishaji wa mazalia ya uhalifu umewekwa kisheria ili kuifundisha jamii kuwa, uhalifu hauna faida na adhabu za kifungo hazitoshelezi kutokomeza uhalifu hasa katika makosa ya kupangwa ikiwemo makosa ya dawa za kulevya. Huu ni mkakati wa kuzuia uhalifu kuendelea na kuondoa matamanio ya kufanya uhalifu.
Orodha ya mali zilizotaifishwa ni:
1. Apartment Namba OA2, Ghorofa ya Kwanza, iliyopo Sea Breeze Residential Complex, kiwanja Namba 192
Block "O", Jangwani Beach, Kinondoni, Dar es Salaam.
2. Apartment 6B, kiwanja Namba 26 Block 52, iliyopo Kariakoo, Ilala, Dar es Salaam.
3. Nyumba iliyo kwenye kiwanja Namba 329 na 1009 Block "C", Mbezi wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.
4. Kiwanja Namba 69 Block 7, kata ya Mbweni JKT, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
5. Nyumba Namba 14, iliyopo kiwanja Namba 131 Block 9, mtaa wa Chui Mtoni Kijichi, NSSF House Scheme
Phase III, Temeke, Dar es Salaam.
6. Kiwanja Namba 44768, kilichopo mtaa wa Kigogo kata ya Kisarawe II, Kigamboni Dar es Salaam.
7. Kiwanja kilichopo Shungubweni Village, kata ya Shungubweni, wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani.
8. Kiwanja Namba 53 Block E, Boza Village, Wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani.
9. Kiwanja kilichopo Boza village, kata ya Boza wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani.
10. Kiwanja Namba 8 Block C, kilichopo mtaa wa Mwambao, kata ya mji Mkongwe, wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani.