Lavit
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 14,834
- 32,522
1. Gari ni kama nguo liendeshe wewe tu. Usimpe mtu hata kama ni ndugu yako. Akanunue Lake.
Nakazia
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
1. Gari ni kama nguo liendeshe wewe tu. Usimpe mtu hata kama ni ndugu yako. Akanunue Lake.
Ni wivu tu.Unakuta mtu yupo yupo tu lakini basics za barabarani hajui hata kidogo. Mtu ameblock barabara na wala haoni shida.
Mtu amekukuta umepaki sehemu anakuja kukublock ushindwe kutoka mpaka umuite! Mbaya zaidi wakati anapark kulikuwa na nafasi kubwa tu ya kumfanya asikublock.
Inaudhi sana.
Na parking inabidi ziwekewe standards, yaani zile za kukaa muda mfupi na zile za kukaa muda mrefu. Kuna mtu anahitaji parking ya dakika 10 hadi 30. Mwingine atataka kupaki siku nzima so imagine wewe unataka kupaki gari nusu saa halafu anakuja mtu anapaki nyuma yako ila ndio kafika hapo hadi jioni.Kama muhimbili mule ndani baadhi ya maeneno watu wana park hovyo hovyo ushamaliza shughuli zako unafika parking unakuta gari imeblock kutoka haiwezekani inabidi usuburi linakuja jamaa linajichekesha chekesha kuondoa gari yake kama demu
HahahaKwenye funguo za gari kunatakiwa kuwa na kisu. Mengine ukiyataka njoo pm
NATILIA MKAZO HAPAKipengele ambacho watu hukipuuza na ndicho muhimu ni kipengele cha sheria na kanuni za matumizi ya alama, taa, ishara na vielelezo vya barabarani.
Hapo ndipo huwa wengi wanapotea. Kuendesha gari ni asilimia ndogo sana ya udereva. Dereva mzuri ni yule anayejua sheria za barabarani vema na mwalimu mzuri kwa wenzake.
Hata kama lesenj yako uliipata kimagumashi, hebu kuwa mzalendo kwa kujifunza sheria za barabarani na alama zake kwa umakini, zingatia kujifunza mabadiliko ya alama za barabarani maana kuna vitu vipya vinatokea kama zile njia za kule Kimara ambazo mzunguko wake ni tofauti sana na mizunguko ya mataa ambayo madereva wamezoea so kutia boko ni rahisi.
So ni wajibu wako kama muendesha chombo cha moto kutenga muda wakusoma na kujifunza sheria za barabarani na usiishie hapo tu aanza kuelewa na culture ya madereva wa Tanzania. Mfano, sheria inasema katika foleni umaintain distance ya mita 1 kama sio 3 kati ya gari yako na ya mbele yako kiusalama but ukiacha hiyo distance daladala na IST zitakuchomekea sana.