Kipengele ambacho watu hukipuuza na ndicho muhimu ni kipengele cha sheria na kanuni za matumizi ya alama, taa, ishara na vielelezo vya barabarani.
Hapo ndipo huwa wengi wanapotea. Kuendesha gari ni asilimia ndogo sana ya udereva. Dereva mzuri ni yule anayejua sheria za barabarani vema na mwalimu mzuri kwa wenzake.
Hata kama lesenj yako uliipata kimagumashi, hebu kuwa mzalendo kwa kujifunza sheria za barabarani na alama zake kwa umakini, zingatia kujifunza mabadiliko ya alama za barabarani maana kuna vitu vipya vinatokea kama zile njia za kule Kimara ambazo mzunguko wake ni tofauti sana na mizunguko ya mataa ambayo madereva wamezoea so kutia boko ni rahisi.
So ni wajibu wako kama muendesha chombo cha moto kutenga muda wakusoma na kujifunza sheria za barabarani na usiishie hapo tu aanza kuelewa na culture ya madereva wa Tanzania. Mfano, sheria inasema katika foleni umaintain distance ya mita 1 kama sio 3 kati ya gari yako na ya mbele yako kiusalama but ukiacha hiyo distance daladala na IST zitakuchomekea sana.