Inasikitisha sana, tuliomba kuunganishiwa maji mwezi wa 7 mwaka 2023. Control number tukapewa mwezi wa 3 mwishoni baada ya kutoa malalamiko yaani control number imechukua miezi 8 kuipata.
Sasa tumelipia kuunganishiwa maji tarehe 7 mwezi wa 4 hadi muda huu siku 7 za mkataba wa kuunganishiwa maji zimekwisha hamna dalili ya kuhudumiwa.
Ni takribani miezi 10 mpaka sasa tangu tangu tufanye maombi ya kuunganishiwa maji lakini hatujaambulia kitu. Wanadai vifaa hakuna bila hata kujiuliza hivyo vifaa mteja anahisikaje?!
Nimepanga kupeleka malalamiko wizara husika pamoja na takukuru. Ili haki na uwajibikaji uchukue mkondo. DAWASA ni bomu lingine ni wazembe sana.