KERO Mamlaka ya Maji Mtwara hukata maji mchana na kuyafungulia usiku wa manane

KERO Mamlaka ya Maji Mtwara hukata maji mchana na kuyafungulia usiku wa manane

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kumekuwa na utaratibu mbovu wa mamlaka ya maji Mtwara (MTUWASA) kukata maji mchana na kuyaachia usiku wa manane muda ambao Wananchi tumelala, hali ambayo inatufanya badala ya kupumzisha mwili tunaanza kufanya kazi ya kukesha kusubiri maji kisha kukikucha tena tunaingia mtaani kusaka hela.

Hii kadhia tumedumu nayo kwa zaidi ya miezi 6. Tunaomba mamlaka husika kufanyia kazi kadhia hii.

Maeneo mengi yamekuwa yakiathiriwa na changamoto hiyo kiasi cha kusababisha hata miradi kadhaa nayo kusua sua kwa kuwa hakuna maji ya uhakika.

Baadhi ya maeneo ambayo yanaathiriwa zaidi na hali hiyo ni maeneo ya Mtwara mjini ikiwemo Coco Beach, Shangani na Ligula.

Serikali inatakiwa kuingilia suala hili kwani linatuumiza wengi na kuharibu ratiba nyingi za Kijamii na kiuchumi.

Pia soma ~
MTUWASA: Mahitaji ya maji Manispaa ya Mtwara Mikindani ni makubwa kuliko uzalishaji ambao ni 63%
 
Back
Top Bottom