One bisacka
New Member
- Aug 30, 2026
- 1
- 0
Mamlaka ya Maji Sengerema (SEUWASA) imekuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa za kiutendaji na kifedha, hali ambayo imeanza kuwaathiri sana watumishi pamoja na utoaji wa huduma kwa wananchi.
Kwa mujibu wa hali tunayoiona katika taasisi, kuna changamoto kubwa ya upatikanaji wa fedha za kuendesha shughuli za kila siku. Taasisi inadaiwa katika maeneo mbalimbali, ikiwemo umeme, mafuta na madawa, huku baadhi ya magari ya taasisi yakiwa mabovu na yameshindwa kufanya kazi.
Hali hii pia imeathiri maendeleo ya watumishi. Tunashindwa kupandishwa madaraja kwa wakati kutokana na kukosekana kwa bajeti, jambo linalokatisha tamaa watumishi ambao wanatekeleza majukumu yao licha ya mazingira magumu ya kazi.
SEUWASA pia imebaki kuwa moja ya mamlaka za maji za wilaya zinazofanya kazi ndani ya Mkoa wa Mwanza, wakati wilaya nyingine zimeunganishwa chini ya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Mwanza (MWAUWASA).
Tunaomba mamlaka zinazohusika zifanye uchunguzi wa kina kuhusu hali ya kifedha na kiutendaji ya SEUWASA, na zitafute suluhisho la haraka ili kuhakikisha taasisi inaweza kujiendesha, watumishi wanapata stahiki zao na wananchi wanaendelea kupata huduma bora za maji.
Tunaomba msaada na hatua za haraka kabla hali haijawa mbaya zaidi.