A
Anonymous
Guest
Mamlaka ya Huduma ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Wilaya ya Musoma, Mkoa wa Mara, imeshindwa kutoa huduma ya maji kwa wananchi wake kwa kipindi cha zaidi ya wiki mbili sasa.
Wananchi wa kata za Buhare, Rwamlimi na Nyakato wameathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na ukosefu wa huduma hiyo muhimu, huku mamlaka husika ikishindwa kutoa taarifa ya wazi kuhusu chanzo cha tatizo hilo na muda wa kurejesha huduma.
Tunaomba Mamlaka ya Maji Musoma itoe ufafanuzi kwa wananchi kuhusu sababu za kukosekana kwa maji kwa muda mrefu kiasi hicho. Je, tatizo ni nini hasa, na ni hatua gani zinachukuliwa kuhakikisha huduma ya maji inarejea haraka?
Soma Pia: Wiki tatu bila maji: Wananchi wa Unyinga, Mamise na Unyakumi tunataka ufafanuzi kutoka SUWASA
Wananchi wanahitaji taarifa sahihi na huduma bora kwa kuwa maji ni hitaji la msingi la maisha ya kila siku.