Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 417
Mamlaka ya Mapato Uganda imemtaka aliyekuwa mgombea wa upinzani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 nchini Uganda, Robert Kyagulanyi, Bobi Wine, kurudisha gari lake jipya alilonunua ambalo haliruhusu kupenya risasi, ikisema gari hilo liliruhusiwa mpakani kimakosa
Mapema juma lililopita, Bobi Wine aliwaambia wafuasi wake kuwa amefanikiwa kununua gari aina ya Toyota Land Cruiser V8 baada ya kukusanya michango ya wafuasi wake ndani na nje ya Uganda, na lilikuwa aina ya gari lisiloruhusu kupenya kwa risasi. Hii ilikuwa baada ya Mamlaka ya Mapato kutoa kibali kwa gari hilo na kumruhusu Bobi Wine kulitumia.
Sasa URA inasema kuwa thamani ya gari hilo ni kubwa kuliko ile iliyoandikwa awali, ikimtaka Bobi Wine kulirudisha gari kwa Mamlaka hiyo ili kuangaliwa upya. URA imedai kuwa hakukuwa na taarifa kuwa gari hilo lilikuwa haliruhusu kupenya risasi wakati wa usajili.
Mamlaka hiyo inadai kuwa thamani ya gari iliyosajiliwa ni takriban Sh milioni 158 za Uganda (sawa na Tsh milioni 100) hivyo ushuru wake ulikuwa Sh milioni 88 (sawa na Tsh milioni 55), ikitaka kurudishwa kwa gari hilo ili kuhakikisha thamani yake upya.
Hatua hiyo ya Mamlaka imemkasirisha Robert Kyagulanyi, ambapo mwanasheria wake, Anthony Wameli, ameiandikia barua Mamlaka hiyo akidai kuwa hatua hiyo ni kinyume na sheria na inamnyima mteja wake haki ya kumiliki mali.
Hata hivyo, Mamlaka ya Mapato imesema kuwa kumtaka Wine kurejesha gari ili kulifanyia ukaguzi upya ni jambo la kawaida.
Utafiti wa mtandao wa intaneti unaonesha kuwa gari jipya aina ya Toyota Land-Cruiser V8 inagharimu kuanzia dola elfu 85 (sawa na Tsh. Milioni 197) lakini aina hiyo hiyo ya gari linalozuia risasi kupenya hufikia dola 395,000 hadi 450,000 (sawa na Tsh. milioni 917 hadi bilioni 1).
Chanzo: Daily Monitor