Upekuzi101
JF-Expert Member
- Aug 28, 2020
- 221
- 542
Salam wana JF.
Nina matumaini yangu wote mpo salama. Napenda kuwaeleza juu utendaji dhaifu wa mamlaka ya Ngorongoro. Jana jioni magari mawili (fuso 1 na basi 1) yalikwama na kufunga barabara, iliyopelekea wageni waliokuwa wanataka hifadhi ya Serengeti kuelekea, Ngorongoro crater, Karatu na Arusha kushindwa kupita.
Hii imepelea wageni kuchelewa ndege kwa wale waliokuwa wanasafiri kwa siku ya jana na wale waliokuwa wanakuja Arusha kuchelewa sana kufika. Kinachosikitisha zaidi ni namna hili swala lilivoshungulikiwa, grader ya Kuja japo kusogeza hayo magari ili kufungua njia ilichelewa kufika sana, na ilipofika muda ulikuwa umeenda kidogo hata uendeshaji wa mashine hiyo ukawa mgumu hadi kupelekea nayo kukwama kitu kilichopelekea adha na usumbufu usiokuwa wa msingi ukizingatia umbali ilipo ofisi na sehemu walipokwamia wageni ni karibu kiasi kuwa kama umakini ungekuwepo hili swala lingeisha mapema.
Swala kama hili linaleta mashaka na maswali mengi hasa kwenye taasisi za serikali kama kweli wapo tayari kukabiliana na majanga. Sote tuliona zoezi la uzimaji moto Kilimanjaro lilivoenda kwa kusuasua huku Tanapa na mamlaka Ngorongoro vikiwa vinachangia kipato kikubwa kwenye uchumi wa nchi.
Sote tuliona ajali ya ndege ilivotokea Mwanza hali ilivyokuwa na namna zoezi la ukoaji lilivofanyika katika hali ya kuzorota na kutia hasira.
Rais SSH una changamoto kubwa Sana hasa kwa viongozi na wakuu wa vitengo vya usalama na ukoaji, hasa kwenye hifadhi za taifa na maeneo mengi ukizingatia utendaji kazi haswa kwenye majanga na uokozi kushindwa kutimiza majukumu yao.
Kama udhaifu upo kwenye Serikali yako kushindwa kuwawezesha kufanya kazi yao, basi waweze vifaa vya uokozi maana ni aibu mlima kuungua week 2 nzima bila kuwa hata na ndege moja ya kuuzima moto ukizingatia idadi ya mbuga na vivutio tulivyonavyo.
Tujaribu kufikiri kidogo siku Serengeti ikiwaka moto, Ruaha ikawaka moto, Kilimanjaro ikawa inawaka moto, je Tanzania Ina nguvu na uwezo wa kupambana na iyo hali.
Mwisho kabisa mama ondoa wazwmbe wote wanaokuongezea mzigo kwenye kazi yako, alafu waangalie sana viongozi wanaokusifia sifia na kukwambia unaupiga mwingi kukuzuga wakati wao ndo wanakufelisha.