Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
NAIBU WAZIRI ATUPELE MWAKIBETE AKABIDHI VYETI KWA MADEREVA 999 KUTOKA LATRA
Naibu Waziri Uchukuzi na Ujenzi, Mhe. Atupele Mwakibete tarehe 01 Julai, 2023 jijini Dar es Salaam ametoa vyeti kwa madereva 999 waliosailiwa na kuthibitishwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini Nchini (LATRA), hii ni katika kuhakikisha usalama wa watumiaji wa vyombo vya moto ili kuwe na uhakika wa usalama na kupunguza matukio ya ajali za barabarani.
Hafla ya ugawaji vyeti imefanyika Jumamosi Julai 1, 2023 katika Ukumbi wa Arnaoutoglou Wilaya ya Ilala na kufunguliwa na Mhe. Atupele Mwakibete (MB), Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi)
Hafla ya ugawaji vyeti imefanyika Jumamosi Julai 1, 2023 katika Ukumbi wa Arnaoutoglou na kufunguliwa na Mhe. Atupele Mwakibete (MB), Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi)
"Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuiwezesha LATRA kutekeleza majukumu yake ambayo ni muhimu na kwa mujibu wa sheria" - Mhe. Atupele Mwakibete, Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi
"Vyeti hivi vitatambulika kitaifa na kimataifa na hasa kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Soko la pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) na Jumuiya ya Maendeleo ya NchiKusini mwa Afrika (SADC)" - Mhe. Atupele Mwakibete, Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi
"Nawapongeza sana LATRA kwa kuendelea kushirikiana na taasisi nyingine za umma ikiwemo Jeshi la Polisi, Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na VETA kwa kuandaa kwa pamoja maswali yenye nia njema ya kufahamu uelewa wa madereva wetu" - Mhe. Atupele Mwakibete, Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi
Aidha, katika hafla hiyo Mhe. Jumanne Sagini, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, amezindua Mitaala ya Mafunzo kwa Wahudumu wa Vyombo vya moto kibiashara.