Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) yaingilia kati mgogoro wa Kampuni ya Bima ya IGT kushindwa kulipa madeni

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) yaingilia kati mgogoro wa Kampuni ya Bima ya IGT kushindwa kulipa madeni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imefafanua juu ya kinachoendelea katika Kampuni ya Insurance Group of Tanzania (IGT) ambapo kuna Watanzania wanaodai kuwa wanaidai Kampuni hiyo lakini imekuwa ikiwazungusha malipo yao kwa miaka kadhaa sasa.

Awali andiko la Mwanachama wa JamiiForums.com lilieleza kuwa baadhi ya watu wanaoidai Kampuni hiyo ya Bima walilazimika kulala ofisini hapo wakishinikiza kulipwa malipo yao ambayo wamedai wamekuwa wakizungushwa kulipwa.

Pia Mdau akadai baada ya kuafikiana kuhusu malipo wakiwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, upande wa IGT imegoma kulipa kwa madai imepata maelekezo mapya kutoka TIRA.

Kusoma zaidi kuhusu madai hayo bonyeza hapa ~ Kampuni ya Bima ya IGT inatuzungusha miaka kutulipa stahiki zetu, tumeamua kulala ofisini ili tulipwe
photo_2024-08-05_10-45-42.jpg
Mmoja wa wanaoidai Kampuni ya IGT akiwa amelala ofisini hapo katika njia ya kushinikiza kulipwa.

UFAFANUZI WA MAMLAKA YA BIMA
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Hadija Maulid anaelezea:

TIRA haijazuia malipo, ilichofanya ni kutimiza taratibu kwa mujibu wa Sheria hasa pale Mamlaka inapoona Kampuni ina changamoto, Kamishna wa Bima Tanzania ana mamlaka ya kuteua Meneja wa Muda (Statutory Manager) ambaye anasimamia utendaji kwa jumla.

Uwepo wa Meneja huyo unaendana na mabadiliko mengi ikiwemo mabadiliko ya Watu wanaosaini katika masuala ya Uhasibu, hivyo kwa wiki hii kutakuwa na changamoto ya malipo lakini kitakachofuata watalipwa vizuri zaidi kwa kuwa utaratibu utakuwa vizuri mzuri.

Moja ya majukumu ya TIRA ni kusimamia Wabima wapate haki yao, wanaokata Bima wanatakiwa kulipwa kulingana na soko lilivyo, Bima ni kitu cha msingi na wateja lazima wawepo.

Taarifa juu ya jambo hilo ilitolewa na wanaohusika walijulishwa.

Kuhusu madai kuwa TIRA imekuwa ikiingilia kila mwaka linapofika suala la malipo sio kweli, Meneja wa Muda ameweka kipindi hiki katika kampuni hiyo.

Unajua inapotokea hali kama hiyo TIRA lazima iangalie kwanini kampuni inayumba na inashindwa kujiendesha na je madeni na malipo yanayofanyika yanakuwa na uhalisia

Meneja huyo wa Muda ataangalia kila kitu kinachoendelea na kujua nini hasa kimesababisha uwepo wa changamoto hiyo inayoendelea
 
Back
Top Bottom