Mamlaka Ya Vitambulisho Vya Taifa Nida Tumieni Teknolojia Kurahisisha Upatikanaji wa Huduma Kwa Jamii

Joshua Mbezi

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2024
Posts
1,994
Reaction score
4,446
Baadhi ya wananchi wamekumbana na changamoto ya kufungiwa namba zao za Nida kwasababu ya kutokuchukua kadi zao za Nida. Tatizo hili limesababishwa na serikali yenyewe kwasababu imekuwa ikitumia muda mrefu kutoa Vitambulisho na wananchi wengi kutokana na harakati za utafutaji wamejikuta wakihama sana.

Kwa mfano mtu alijiandikisha mwaka 2019 akiwa Mtwara namba na kitambulisho vinatoka akiwa tayari amehamia mkoa mwingne mfano Kagera nauri ya kutoka Kagera kwenda Mtwara si chini ya Tsh 300k

Je, mtu huyu anasaidiwaje kupata kadi yake na ikiwa hana ndugu yeyote wa kumchukulia kadi yake kule Mtwara?

Ila ingekuwa rahisi kama Mamlaka Ya Vitambulisho Vya Taifa Nida wangekuwa na Huduma ya online soft copy mtu angeingia kwenye website yao Kisha kupakua kitambulisho chake na kwenda ku print stationary au ata kwenye ofisi yoyote ya Nida iliyo karibu yake
Suala la kufungia namba hatutatui tatizo Bali ni kuongeza tatizo
Lakini pia wanaweza kutumia mfumo wanaoutumia Tume Huru ya Uchaguzi

Mfumo wa kupitia mkoa mmoja baada ya mwingne na kuwasajiri Wananchi wote waliokidhi vigezo na kuwapatia Vitambulisho vyao ili kuondoa mrudikano wa Vitambulisho ofisini na kuzuia mianya ya rushwa.

Maana mfumo unaotumika kwa sasa unawafanya maofisa Nida pamoja na maofisa uhamiaji kuomba rushwa sana kwa wananchi
Waziri wa Mambo Ya ndani Mh Innocent Bashungwa fanya namna ya kumalizq tatizo hili maana linawatesa sana wananchi.
 
Kama hapa mjini Kuna watu wameandikisha tokea mwaka 2021 mpaka Leo hawajapata sembuse huko kijijini nyuma umya TV , Mamlaka zimefeli.
 
Back
Top Bottom