Responded HOJA Mamlaka za afya zichukue hatua za haraka sana kuzuia aina hii ya kuandaa chapati kwa kutumia sponji

Responded HOJA Mamlaka za afya zichukue hatua za haraka sana kuzuia aina hii ya kuandaa chapati kwa kutumia sponji

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

Vien

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2020
Posts
8,508
Reaction score
15,276
Habari wakuu,

Kumekuwa na mtindo mpya wa kuchoma chapati nyingi kwa wakati mmoja kwenye 'maframpeni' makubwa sehemu za migahawa mikubwa ili kuweza kukidhi huduma kwa wateja kwa haraka.

Lakini kutumia sponge (yako kama godoro) katika utengenezaji inaharatarisha afya ya mtumiaji kwakuwa particle ndogo ndogo zinazoingia kwenye chapati zinaweza kuleta cancer.

Nilishawahi kuleta huu uzi kipindi cha nyuma kidogo, lakini naona hili swala ndo limeshika kasi sana, swala lenyewe ni huu uandaaji wa chapati kwa kutumia sponji, ukienda migahawa mingi, watu wanatumia sponji kwenye uchomaji wa chapati kwakua inasaidia sana kuweza kurahisisha, lakini tukirudi kwenye afya ya mlaji ni hatari mnoo, kwani zile chembe ndogo ndogo za sponji nazo zinaungua pamoja na chapati, matokeo yake walaji wanakua na hatari kubwa ya kupata canser

Soma pia > Kukaanga Chapati kwa kutumia Sponji daktari Koshuma asema magodoro ya kisasa yanatengenezwa kwa povu lenye kemikali za viwandani
 
Maji ya chupa nayo huwa na vichembechembe vidogo sn vya chupa tunavinywa.
Kiufupi mambo ni mengi sana yanayohatarisha afya zetu hasa kupitia vyakula.
 
Ila soda za viwandani mnakunywa. Na mmepunguziwa kodi kwenye energy drink mnywe vizuri. Ukiona sponji kwako sio nzuri, usile hizo chapati kama sisi ambavyo hatunywi energy drink.

Hata hivyo biashara ndogo ndogo za vyakula sio salama kwa afya ya mlaji. Ugali wanaweka kwenye mifuko ya plastic/nylon ili usipoe, migahawa ipo barabarani vumbi tupu. Kikubwa chagua unapoona ni salama kwako.
 
Habari wakuu,

Nlishawai kuleta huu uzi kipindi cha nyuma kidogo, lakini naona hili swala ndo limeshika kasi sana, swala lenyewe ni huu uandaaji wa chapati kwa kutumia sponji, ukienda migahawa mingi, watu wanatumia sponji kwenye uchomaji wa chapati kwakua inasaidia sana kuweza kurahisisha, lakini tukirudi kwenye afya ya mlaji ni hatari mnoo, kwani zile chembe ndogo ndogo za sponji nazo zinaungua pamoja na chapati, matokeo yake walaji wanakua na hatari kubwa ya kupata canser

Nimekuwekea uzi hapo chini 👇🏻

Energy drinker wamewaondolea kodi mfe sawa sawa, mimi nawawlewa sana CCM jinsi ya kucheza ba akili za wajinga wa hii Jamhuri
 
Back
Top Bottom