Mamlaka za China zaweka mazingira maalum kwa ajili ya maisha ajili ya wazee

Mamlaka za China zaweka mazingira maalum kwa ajili ya maisha ajili ya wazee

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
1733124002267.png

Takwimu za mwaka 2022 kutoka Wizara ya Mambo ya Kiraia ya China zinaonesha kuwa idadi ya wazee nchini China, yaani watu wenye umri wa miaka 60 na zaidi, imefika zaidi ya milioni 208.04, ikiwa ni karibu asilimia 20 ya wachina wote. Kutokana na maendeleo ya kiuchumi, kisayansi na teknolojia, umri wa kuishi kwa wachina kwa sasa umefikia wastani wa miaka 78.2. Kwa makadirio ya takwimu za sasa, hadi kufikia mwaka 2050 idadi ya wazee nchini China itakuwa imefikia asilimia 40 ya watu wote nchini China.

Ongezeko hili la idadi ya wazee limeongeza mahitaji ya huduma na matunzo kwa wazee. Kwa sasa mahitaji ya kila siku kama vile chakula na matunzo kwa wale ambao miili yao haina nguvu tena ya kujitunza, ni jambo linalopewa kipaumbele. Kwa wale ambao bado wana nguvu, nao pia wana mahitaji kama vile elimu, kwa wale waliokosa wakati wa ujana wao, na pia burudani.

Hivi karibuni kundi la waandishi wa habari wa ndani na nje ya China lilitembelea eneo moja katika mji wa Yanji wa wilaya inayojiendesha wa kabila la wakorea ya Yanbian, Mkoani Jilin. Kwenye eneo hilo ambalo wakazi wake wengi ni watu wa kabila la wakorea, kuna wazee ambao wanafurahia mipango na juhudi za serikali katika kuwasaidia wazee kuishi maisha yenye furaha. Kwenye kituo cha eneo moja la makazi la Danying, kuna wazee ambao wanajumuika kwa ajili ya michezo ya ngoma za jadi, chesi ya jadi, michezo mbalimbali ya bao, sanaa ya uandishi wa maandiko ya jadi ya kichina (calligraphy) na wengine wanashiriki kwenye mambo ya upishi.

Kauli mbiu ambayo imekuwa inafuatwa na mamlaka za eneo hilo katika kushughulikia mambo ya wazee ni “furaha imefika”, ikiwa na maana kuwa baada ya kufanya kazi wakati wa ujana, uzeeni ni wakati wa kupumzika na kufurahia maisha. Mkoa wa Jilin, uko kwenye eneo lenye baridi kali sana nchini China, ambalo wakati wa baridi, baridi hufikia zaidi ya nyuzi 20 chini ya sifuri. Baridi kali ni moja ya changamoto kubwa kwa wazee, lakini kituo kitu cha burudani kwa ajili ta wazee kimezatitiwa kwa mfumo wa joto, ambao huwafanya wazee wote waliondani yake wafurahie burudani bila kuwa na wasiwasi.

Pamoja na kuwa maeneo ya mpakani yanatajwa kuwa ni maeneo ya mbali ambayo maendeleo hufika polepole ikilinganishwa na maeneo ya mengine kama ya pwani, katika wilaya ya Yanbian maendeleo yanaonekana katika nyanja nyingi. Iwe ni miundo mbinu ya kisasa ya barabara, au makazi bora kwa wenyeji, na hata kwenye shughuli mbalimbali za kijamii. Wazee wa maeneo hayo wanaweza kupata huduma mbalimbali zinazofanana na zile za wakazi wa mijini.

Changamoto ya ongezeko la idadi ya wazee nchini China iko wazi kabisa, hata hivyo mfano unaonekana katika mji wa Yanji, unaonesha kuwa hatua mbalimbali zilozoanza kutekelezwa, zinaonesha kuwa sera zinazozingatia hali na mazingira ya kila eneo, hatua kwa hatua zinahakikisha wazee wa China wawe na maisha ya uzee yenye.
 
Back
Top Bottom