- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Kumekuwepo na chapisho lililosambazwa kwenye mtandao wa Facebook, kupitia ukurasa wa Nalinga Media, na baadhi ya tovuti za kimatifa likidai kuwa mamlaka za Iran zimegundua fuvu la kichwa cha askari wa Jeshi la Marekani katika eneo la Isfahan, katikati mwa Iran.
Chapisho hilo linaeleza kuwa fuvu hilo lilipatikana miongoni mwa mabaki ya ndege ya kijeshi ya Marekani iliyodaiwa kudunguliwa wakati wa mapigano ya hivi karibuni kati ya Marekani na Iran.
Chapisho hilo linaeleza kuwa fuvu hilo lilipatikana miongoni mwa mabaki ya ndege ya kijeshi ya Marekani iliyodaiwa kudunguliwa wakati wa mapigano ya hivi karibuni kati ya Marekani na Iran.
- Tunachokijua
- Kumekuwepo na chapisho lililosambazwa kwenye mtandao wa Facebook, kupitia ukurasa wa Nalinga Media, na baadhi ya tovuti za kimatifa likidai kuwa mamlaka za Iran zimegundua fuvu la kichwa cha askari wa Jeshi la Marekani katika eneo la Isfahan, katikati mwa Iran.
Chapisho hilo linaeleza kuwa fuvu hilo lilipatikana miongoni mwa mabaki ya ndege ya kijeshi ya Marekani iliyodaiwa kudunguliwa wakati wa mapigano ya hivi karibuni kati ya Marekani na Iran.
Uhalisia wa madai hayo ni upi?
kwa kutumia nyenzo ya ufuatilaji wa maneno mhimu (keyword search ) kwenye mitandao ya kidijitali unaonyesha kuwa hakuna uthibitisho wowote wa kuaminika unaonyesha kuwa jeshi la Iran limegundua fuvu la kichwa cha mwanajeshi wa Marekani.
Aidha, vyombo vikuu vya habari vya Iran kama Tasnim News Agency, IRNA na Press TV havijachapisha taarifa inayothibitisha madai hayo. Badala yake, vyombo hivyo viliripoti kuwa Iran imedai kuharibu ndege kadhaa za kijeshi za Marekani, zikiwemo ndege ya usafirishaji aina ya C-130 pamoja na helikopta za Black Hawk. Tazama hapa na hapa
Hakuna ushahidi wa kuaminika unaothibitisha madai kuwa Iran imegundua fuvu la kichwa cha askari wa Marekani. Vyombo rasmi vya habari vya Iran havijaripoti taarifa hiyo, na kauli ya Rais wa Marekani inaonesha kuwa wanajeshi waliokuwa wakitafutwa wameokolewa wakiwa hai.
Sambamba na hayo, Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kupitia mtandao wake wa Truth Social kuwa wanajeshi waliokuwa wakitafutwa wamepatikana. Katika chapisho lake, alinukuliwa akisema:
"TUMEMPATA! Ndugu zangu Wamarekani, katika saa chache zilizopita, Jeshi la Marekani limefanikisha moja ya operesheni za utafutaji na uokoaji za ujasiri zaidi katika historia ya Marekani.
Mwanajeshi huyu jasiri alikuwa nyuma ya mipaka ya adui katika milima hatari ya Iran. Alipata majeraha, lakini atakuwa mzima kabisa.Operesheni hii ya ajabu ya utafutaji na uokoaji imekuja sambamba na mafanikio ya uokoaji wa rubani mwingine jasiri, siku iliyopita".