Mpaka sasa haijajulikana ana kosa gani kwani hajafikishwa mbele ya chombo chochote cha sheria na pia wana Ngara hawakuwahi kusikia uhalifu ama kosa lake kokote kule zaidi ya misimamo yake ya kupingana na matendo yasiyofaa, kutoa mawazo yake na kutetea maslahi ya Wananchi.
Kijana huyu ambaye amezaliwa kijiji cha Nyamagoma, na kuhitimu Shahada yake ya Kwanza ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) Mwanza amekuwa chachu ya siasa za Ngara kwa kiasi kikubwa kupitia mijadala yake na misimamo yake yenye utata.
Ni Rai yangu kwa vyombo vya Dola Ngara na Kigoma kuweka nguvu ya pamoja kumtafuta Kijana huyu na ikiwezekana kuwawajibisha watakaobainika kuhusika na Utekaji huu kwani unalenga kuchafua taswira ya Tanzania katika nyanja ya Usalama.