Mamlaka za Zanzibar (DCEA) imekamata dawa za kulevya zilizofichwa kwenye pipi, chocolate, korosho na shisha

Mamlaka za Zanzibar (DCEA) imekamata dawa za kulevya zilizofichwa kwenye pipi, chocolate, korosho na shisha

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Zanzibar (DCEA), kwa kushirikiana na Kikosi Kazi cha Uhalifu wa Kupangwa Zanzibar (ZTOCTF), imebaini mbinu mpya zinazotumiwa kusafirisha dawa za kulevya kwa kuzificha ndani ya bidhaa za kawaida zinazotumiwa na wananchi kila siku.

Katika operesheni maalum, maofisa walikamata pipi, chokoleti, korosho na bidhaa za shisha zenye majina ya ELF Bar na Freshy ambazo zilikuwa na dawa za kulevya zikiwemo bangi, cocaine na Lysergic acid diethylamide (LSD), zikiwa na uzito wa jumla wa kilo 7.448.

Ukamatwaji huo unaonesha jinsi wahalifu wanavyoendelea kubadili mbinu zao kwa kutumia vyakula na bidhaa za burudani zinazoonekana za kawaida kusambaza dawa za kulevya, wakilenga zaidi watoto walio chini ya umri wa miaka 18 na vijana ambao ndio tegemeo la taifa.

Bidhaa hizo zilikuwa zikiuzwa katika maduka yaliyotajwa kuwa ni Popeyes UK Treatz na Shop N’GO katika maeneo ya Unguja Kusini na Magharibi, hususan Paje, Jambiani, Mbweni na Shangani, pamoja na ghala lililopo Mpendae.

Akizungumza na waandishi wa habari Jumatatu, Machi 2, 2026, Kamishna wa Mamlaka hiyo, Kanali Burhani Zuberi Nassor, alisema operesheni hiyo ilifanyika kwa siku mbili, Januari 25 na 29.

1772453151374.png

Chanzo: The citizen
 
Back
Top Bottom