robert christian
New Member
- Apr 30, 2026
- 1
- 1
Mimi ni mmiliki wa gari binafsi na mkazi wa Manispaa ya Ubungo. Wiki mbili zilizopita nilifika maeneo ya Manispaa ya Kinondoni kwa gari langu, na tangu siku hiyo nimekuwa nikikuta kwenye mfumo wa tozo za maegesho kwamba ninadaiwa Sh500, huku eneo likioneshwa kuwa ni Kinondoni Municipal.
Tatizo ni kwamba sijawahi kuegesha gari katika eneo hilo. Nilipouliza baadhi ya watumishi wanaokusanya tozo kwa njia ya kielektroniki, nilielezwa kuwa kuna uwezekano gari kupigwa picha kwa simu na taarifa zake kuingizwa kwenye mfumo, jambo linaloweza kusababisha udanganyifu.
Naomba mamlaka husika kuboresha mfumo wa tozo za maegesho, ikiwemo kuhakikisha mmiliki anapopangiwa tozo anapokea ujumbe kwenye simu papo hapo, ili aweze kuthibitisha kama tozo hiyo ni halali au la.