A
Anonymous
Guest
Mimi ni mtumishi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete [JKCI], taasisi hii inatupa wakati mgumu watumishi wake kupitia bosi wetu,
Lakini kabla ya kufika kwa bosi kubwa, kuna watu hapo chini yake awanatumia nafasi vibaya kwa kuingiza wao wao kwenye mifumo ya ajira kinyume cha utaratibu, huku baadhi ya wanaojitolea na wanaofanya kazi kwa mkataba wakiwa hawapati nafasi hizo.
Ipo hivi, kuna muda nafasi za ajira zinatolewa na Serikali, wao mabosi waliopewa nafasi kusimamia wanapendekeza watu wao ambao wengine hata hawapo hapo katika taasisi wanawaingiza kwenye mapendekezo ili wapate ajira, wale vijana waliopo wanaojitolea na wengine wa mkataba wao wanabaki kama walivyo, hiyo yote ni kwa kuwa bosi kubwa hana muda wa kufuatilia.
Nije kwa bosi kubwa mwenyewe huyu kiongozi huwa anafokea watumishi mbele ya wagonjwa, hajali kuwa sisi pia ni waajiriwa na tunahitaji heshima.
Pili, anafanya maamuzi ya ghafla bila kushirikisha watumishi, JKCI ina Kurugenzi 6 na vitengo vingi tu, sasa ili uwe kiongozi inapaswa uwe angalau una bachelor degree ktk muundo wa taasisi yetu hii.
Ajabu ni kuwa yeye utaratibu huu haufuati, kamteua mke wake ambaye ana Diploma ya uuguzi na sio Bachelor degree na kumweka awe ndio Ward In-charge katika kitengo cha VIP, hili linaumiza sana, maana wapo watu wana degree na masters ila wameachwa kwa kumhofia yeye.
Outreach nyingi na semina za kwenda mikoani au nje ya nchi hupitishia kitengo alicho mke wake, watumishi hasa wauguzi hatuendi tena semina au outreach, hili jambo linatuumiza sana sisi watumishi.
Anasema hata tumripoti hatuwezi kufanikiwa kwa lolote. Anatamba kuwa yeye akipiga simu moja tu mtu anaweza kutupwa machokoni huko, hali hiyo inamaanisha Watumishi wafanye kazi kwa uoga na sio kwa moyo, hii sisa wa kwa kuwa hii ni taasisi ya afya, tunacheza na maisha ya watu, kufanya kazi kwa kutishana wakati sisi ni watu wazima si sawa.
Lingine, kuna In charge wa Cardiac Catheterization Laboratory [Cathlab], huyu huwa hafanyi kazi mara nyingi, yeye hupata outreach nyingi kwenda nje ya nchi, ameenda USA, India, UK, Hispania, Thailand, South Africa, China na Kenya seminar ndani ya miaka 2 tu, huko hukaa hata wiki kadhaa.
Mkuu wake hutoa kibali cha ruhusa mtu huyu asafiri kushiriki seminar mbalimbali bila kujali kuwa tupo watumishi wengine katika vitengo vyote. Taasisi kwasasa inaendeshwa kwa hisia na mihemko sana hata Idara ya Human Resources Management sio rafiki tena kwa watumishi wa hali ya chini.
Jambo lingine ni kuwa kuna bosi ameanzisha matawi nje ya muhimbili kama Kariakoo, Oysterbay, Kawe na pia kaingia ubia na hospitali ya Kanisa ya Arusha Lutheran Medical Centre [ALMC].
Hospitali hiyo ya Arusha ilifilisika, ila huyo jamaa anatukata posho zetu kuifufua hospitali hiyo, serikali ipo kimya tu. Maisha yetu yamekuwa magumu mno, tunaomba mtusaidie kupaza sauti. Toka lini hospitali ya Private ibebwe kwa makato ya posho zetu?
Ufafanuzi, soma ~ JKCI yajibu hoja ya kuhusu utendaji wa uongozi wa taasisi hiyo, yasema Sheria, Kanuni na Taratibu vinazingatiwa