Mamlaka zifanyie matengenezo kituo cha daladala Tabata Segerea

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2018
Posts
882
Reaction score
3,337
Miundombinu ya hiki kituo imeharibika kiasi fulani na kutengeneza mashimo makubwa ambayo kwa kipindi hiki cha mvua yanahifadhi maji na kusababisha kero kwa wanaotumia kituo hicho.

Kwanza panapitika kwa shida, usipokuwa makini unaogeshwa maji machafu na daladala au bajaji.

Pia yale mashimo yamechimbika sana kiasi kwamba daladala zinapita kwa shida kwa kugonga chini.

Wahusika wakiangalie kituo hiki kwa roho za huruma waache kuwa wabinafsi.

 
Kituo kilikuwa kizuri kinapendeza wabongo mkakigeuza soko now kipo hoi miundo mbinu yote imechoka vibaya

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Wasimamizi wa kituo hiko, watumie kodi na tozo kufanya ukarabati katika kituo hiko.
 
Tumwambie Nchimbi....pia nei sukari imekuwa 5000 ...yote aambiwe tuko hoiiì
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…