Mamlaka zifuatilie Daladala zinazohatarisha usalama wa Abiria kwa uendeshaji mbovu na Askari hawachukui hatua

Mamlaka zifuatilie Daladala zinazohatarisha usalama wa Abiria kwa uendeshaji mbovu na Askari hawachukui hatua

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Kuna Daladala moja inayofanya safari zake Kijichi Spice kwenda Darajani imekuwa na huduma mbovu kwa Abiria wake na wakati mwingine kutishia usalama wa Watu waliomo ndani ya gari hilo na hata waliopo nje.

Dereva wa daladala hiyo amekuwa akiendesha ovyo kwa kutojali Sheria za Barabarani kiasi kwamba mara kadhaa gari hilo limenusurika kupata ajali iwe ni kwa kutaka kugonga Watu, magari mengine au Miundombinu iliyopo pembeni mwa Barabara.
1734069210404.jpeg
Abiria tumekuwa tukilazimika kupanda kutokana na uhaba wa Daladala zinazofanya kazi katika njia hiyo, pia unapokuwa ndani ya gari lugha za Kondakta na Dereva wake sio nzuri, ukilalamika aina ya uendeshaji wanakwambia “Kama hutaki shuka kapande gari lingine”.
1734069241091.jpeg
Wanafanya hivyo kwa kuwa wanajua kwa uchache wa Daladasla zilizopo njia hiyo lazima utapanda tu gari lao.

Inapotokea Abiria wanalalamika kwa Askari wa Usalama Barabarani kuhusu huduma na uendeshaji wa Daladala hiyo na mengine yenye tabia kama hizo hakuna wanachofanywa kwa maana hakuna hatua inayochukuliwa, inavyoonekana wanajuana.
 
Aisee
Huko si ndio ukitoa alfu 10 kwa nauli wanakuachia unapanda bure....
 
Back
Top Bottom