A
Anonymous
Guest
Ningependa kuwasilisha kero kubwa inayohusu wizi na ukabaji unaoendelea katika maeneo ya Buguruni Rozana na mitaa yake jirani, ikiwemo Pandia Street na Mitungi Street.
Kwa mujibu wa hali inayoshuhudiwa na wakazi na wapita njia, matukio haya huonekana zaidi kuanzia majira ya Saa 5 usiku na kuendelea hadi Alfajiri, Watu wenye pikipiki wamekuwa wakitajwa kuhusishwa na baadhi ya matukio hayo, ambapo wahanga hukabwa au kuporwa mali zao, hasa nyakati za usiku.
Hali hii imekuwa ikileta hofu na wasiwasi mkubwa kwa wananchi, hususan wafanyabiashara, wafanyakazi na watu wanaosafiri usiku. Tunaomba mamlaka husika zichukue hatua za haraka kwa kuongeza doria na ulinzi wa usiku katika maeneo haya, pamoja na kuchunguza na kuwakamata wahusika kwa mujibu wa sheria.
Tunaomba pia wananchi wahamasishwe kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama pale wanapoona vitendo vya uhalifu, bila kujihatarisha..