A
Yaani ndege zinatumwa za kutosha kuleta jeshi kamili yaaniHiyo mitaa waachie akina Makebo wewe hama huko mkuu hupawezi
Ningependa kuwasilisha kero kubwa inayohusu wizi na ukabaji unaoendelea katika maeneo ya Buguruni Rozana na mitaa yake jirani, ikiwemo Pandia Street na Mitungi Street.
Kwa mujibu wa hali inayoshuhudiwa na wakazi na wapita njia, matukio haya huonekana zaidi kuanzia majira ya Saa 5 usiku na kuendelea hadi Alfajiri, Watu wenye pikipiki wamekuwa wakitajwa kuhusishwa na baadhi ya matukio hayo, ambapo wahanga hukabwa au kuporwa mali zao, hasa nyakati za usiku.
Hali hii imekuwa ikileta hofu na wasiwasi mkubwa kwa wananchi, hususan wafanyabiashara, wafanyakazi na watu wanaosafiri usiku. Tunaomba mamlaka husika zichukue hatua za haraka kwa kuongeza doria na ulinzi wa usiku katika maeneo haya, pamoja na kuchunguza na kuwakamata wahusika kwa mujibu wa sheria.
Tunaomba pia wananchi wahamasishwe kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama pale wanapoona vitendo vya uhalifu, bila kujihatarisha..
Umkuja lini mjini mbona haya ya kawaida tangu zama za zama mwanangu?!!Kila siku watoto wa Buguruni wanabuni staili Mpya za kutukaba. Tukiweka hela zetu kwenye M-Pesa, kati ya watano waliokukaba basi Mmoja wakala, utaambiwa taja namba zako za Siri...0153
π π π Ila wajiazali mbele ya ZCO watakula njugu za chuma muda si mrefu... Baada ya mwezi tutegemee Buguruni yote kuwa Shwari.
ZCO alikiwasha Sana enzi za Panya Road chini ya RC Papaa CPA Amos MAKALA
Umkuja lini mjini mbona haya ya kawaida tangu zama za zama mwanangu?!!
Kama anayaweza sasa mbona walalamika?Ila siyo Kwa huyu ZCO brother...uliza Panyaroad wapo wapi?