KERO Mamlaka zimeshindwa kudhibidi Vijana wanaovamia Watu, kuwajeruhi na kupora katika Mitaa ya Tabora Polytechnic College?

KERO Mamlaka zimeshindwa kudhibidi Vijana wanaovamia Watu, kuwajeruhi na kupora katika Mitaa ya Tabora Polytechnic College?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

MeVSMe

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2024
Posts
270
Reaction score
425
Mimi ni Mwanafunzi wa Chuo cha Tabora Polytechnic College ambacho kipo Ipuli, hapa chuoni kwetu pamoja na mitaa ya karibu na hapa kuna kundi la Vijana wanaojiita Mabamzi ambao ukikutana nao barabarani hasa majina ya usiku au jioni badi tambua kazi ipo.

Hawa vijana wamekuwa wakipiga watu mapanga, nondo na vitu vingine vingi kwa lengo la kupora vitu mbalimbali, salama yako ni kukimbia tu.

Wamekuwa wakifanya matukio ya aina hiyo mara kwa mara, wanajeruhi Wananchi wanaopita njia na Wanafunzi wa chuoni hapa wanapokuwa wanatoka kusoma usiku.

Mwezi huu wamempiga kijana mwenzetu wa Chuoni alikuwa akikatiza mtaani akapigwa mpaka kuzimia.

Vijana hao wanaogopesha, tunachojiuliza Tabora ina Askari wengi pia ina Kambi kadhaa za Jeshi lakini matendo ya kiharifu kama hayo yanatokea na hayaonekani kudhibitwa.

Tunajiuliza kwa nini wasifanye msako wa vijana waovu na kuwatia ndani, wanatufanya tunaishi kwa hofu na hakuna hatua zinazochukuwa au Vyombo vya Usalama navyo vinaogopa wahalifu hao.

=================================

Jamii Forums imewasiliana na Waziri wa Ulinzi wa Chuo hicho, Mtiba Chacha amesema:

“Ni kweli hiyo changamoto ipo na imekuwepo kwa muda mrefu, hivi karibuni kuna kijana mmoja alishambuliwa na wahuni hao akashindwa hadi kufanya mitihani yake.

“Tumesharipoti changamoto hii mara kadhaa kwa Jeshi la Polisi lakini hatua zimekuwa hazichukuliwe na Vijana hao wanaendelea kufanya yao na kibaya zaidi wameanza hadi kuingia chuoni nyakati za usiku.

Hivi karibuni kuna mmoja alikamatwa wakati akiiba simu, tunaomba mamlaka zinazohusika situsaidie kwani hali siyo nzuri na hii inaweza kuathiri mwenendo wa masomo na kuwafanya Wanafunzi na Wananchi kwa jumla kuishi kwa hofu.”

Pia soma ~ RPC Tabora: Tunafuatilia taarifa za Wahalifu kuvamia Watu, kuwajeruhi na kupora katika Mitaa ya Chuo cha Polytechnic College
 
Back
Top Bottom