Mamlaka zinasubiri nini kumpa ofa ya Uraia Mayele?

Mamlaka zinasubiri nini kumpa ofa ya Uraia Mayele?

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari!

Kuiga jambo si ujinga, cha muhimu ni kuangalia faida za jambo lenyewe.

US. hawana kuchelewachelewa kwenye suala la kutoa offer ya uraia wa kudumu kwa mgeni anayefanya vizuri. Wakiamini yeye au kizazi chake watafanya makubwa kwa Taifa lao.

Tusipoteze fursa hii ya Mayele. Akipata team huko ng'ambo basi tena itabaki historia.

Apewe offer ya uraia na vi package vyake ili asikatae.

Au mnaona raha kufungwa hovyo?
 
Sasa huyo Mayele ukimpa uraia, si ataishia tu kuwa Mtanzania wa kawaida! Maana hawezi kuichezea Taifa Stars (kama ndiyo malengo yako).

Yaani sheria za FIFA haziruhusu mchezaji kuchezea Mataifa mawili kwa upande wa timu ya wakubwa. Fiston Kalala Mayele ameshaichezea timu yake ya Taifa (DRC) katika mashindano mbalimbali.
 
Back
Top Bottom