KERO Mamlaka ziwasaidie watumishi waliohama kuhamishia taarifa zao walikohamia

KERO Mamlaka ziwasaidie watumishi waliohama kuhamishia taarifa zao walikohamia

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Watumishi waliohama kada mbalimbali wanakutana na usumbufu hasa katika mfumo wa ESS katika kupangilia malengo ya utekelezaji na hivyo kuwa kikwazo katika utendaji kazi wao wa kila siku.

Kwa mujibu wa taratibu za sasa wenye jukumu hili la kuhamisha taarifa za watumishi na mishahara ni OR-TAMISEMI.

Tunawaomba wawasaidie watumishi katika hili ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wao..
 
Sorry hao Watumishi wamehama kwa njia ya Mfumo wa ESS Siyo.,, Naomba Jibu pls
 
Au walihama kimagumashi.

Kwa kubadilishana Mkuu..

ni kwamba TAMISEMI wao ndio wana approve baada ya Afisa Utumishi wa unapotoka kuwa ametuma taarifa zenu huko..

changamoto Approval inakuwa ya kusubiri sana
 
Kwa kuomba uhamisho wa kawaida kwenye mfumo huu, je kuna mtu kafanikisha kuhama
Huu sina hakika sana nadhani mambo hayajakaa sawa..
Changamoto itakuwa ni ile ile mfumo haujawa mwepesi bado
 
Tamisemi wanazingua sana kuhamisha mshahara.. mimi toka mwaka jana hadi leo hawajahamisha, ukienda ofisini kwao wanasema nisuburi tu watahamisha, wakati nashindwa kujaza taarifa ess. [emoji849]
 
Back
Top Bottom