Mamu Meja Kunta (A Love Story)

Mamu Meja Kunta (A Love Story)

Hashpower7113

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
1,353
Reaction score
2,142
Oooh! Mamu! 0oh mamuu! We ndo furaha yangu, ooh Mamu! Nimekosa baby wangu... oh Mamu! Unisamehe mke wangu!
Dah! Utakapoisikiliza ngoma hii kwa mara ya kwanza, na kuhakikishia you won't get enough of it. Haijalishi wewe ni mtu unayependa muziki wa aina gani, nakuhakikishia utaipenda! It is very addictive! Ni Singeli! Ndiyo, Singeli lakini ya aina yake, isiyoisha ladha.

Binafsi sikuwa mpenzi wa aina hii ya muziki lakini katika siku za hivi karibuni nimejikuta nikianza kuwaelewa baadh ya wasanii, weka mbali uhuni wao na mengineyo, sikiliza mashairi, sikiliza melody, hakika utakubaliana na mimi kwamba kuna vipaji na miongoni mwa vipaji vikubwa ambavyo kama vikiendelezwa vinaweza kuja kufanya mapinduzi makubwa, ni huyu dogo, anaitwa Meja Kunta!

Ni mdogo ukimtazama lakini ana melody fulani tamu sana! Hebu maneno yasiwe mengi, sikiliza ngoma hii ambayo katika siku za hivi karibuni imegeuka na kuwa national anthem kwenye kumbi za starehe na siyo uswazi tu, hata ushuani! Si watoto na vijana tu wanaoielewa, hata watu wazima na wazee. Ukiisikiliza, itagusa hisia zako! Warning: It's very addictive! Enjoy!
 
Meja kunta na muddy msanii wanajua sana yaani wana ile singeli ya utofauti sio ile weka weka kata kiunooooooo baharia bakora mbili
Umenena vyema mkuu, wengine wanajua singeli ni kelele kibao na maneno ya kihunihuni, mara sijui bahariaa, wahuniii, zogo tupu!
 
Ahsante mkuu, nilikuwa nausikiasikia tu huu mwimbo sikuwa najua ni nani aliyeimba, thnx sana, mtoto kantia raha huyu jomoon,
 
Ahsante mkuu, nilikuwa nausikiasikia tu huu mwimbo sikuwa najua ni nani aliyeimba, thnx sana, mtoto kantia raha huyu jomoon,
Mkuu na ww jina lako kidogo linaleta tafrani ebwana! Salama lakini
 
Back
Top Bottom