Man City hii sasa sifa, khaaa..!!!

Unstoppable halafu mchanganyiko wake anakufunga kila mchezaji kuanzia beki
Halafu wanapiga pace za counter attack ya kasi sana -hizi modifications za tick taka Pep sijui kazitoa wapi?haiwezekani mpira ana possess yeye, foward wakabia juu yaani wakipoteza mpira strikers wanaukimbiza utadhani wao ni watu wa mwisho
Left &right flank Reheem&Lorey Sane wote wana kasi centre Kelvin Debrune yeye namuita Messi wa EPL anapiga interceptions na akiwa na mpira hapotezi ,aisee Team imekamilika
 
Jamaa anatunyoosha, yani mpaka hivi sasa Everton peke yake ndiye kanusurika kaambulia suluhu, wampe tu kombe lake.Yaani jamaa wakikufunga hauna cha kuongea, maana wanakuzidi kila kitu kuanzia magoli,kona, shot on target, shot off taprget na possession zote zao, labda wewe utawazidi kadi za njano na nyekundu.
 
Hawa jamaa wanachonifurahisha ni kwamba wana spirit ya ajabu sn. Ukiwaangalia dakika ya 80, utafikiri mpira ndo unaanza. The very same spirit wanayokuwa nayo kusaka goli la kwanza, ndo hiyo hyo wanakuwa nayo wanapokufunga goli la 5, hata kama ni dakika ya 88 na wewe hujafunga hata moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…