Man City binafsi naona bado ni timu nzuri hata kaliba ya wachezaji walionao ni mapema kuwapima kwa mechi kubwa na timu kubwa duniani kama Real Madrid siku za usoni tutarajie makubwa kwao.
PSG hawana tofauti na Man City tofauti ni ndogo sana. Don Carlo Ancelotti akiwa kocha wa PSG aliwahi kuambiwa na Al Khelafi kama watatole na FC Porto basi hana kibarua. Don alishangazwa na kauli kwanza aliona hana umuhimu wa kuwa hapo isipokuwa mafanikio yananuliwa. Mpira na uwekezaji wake ni project inayohitaji muda mrefu hayapimwi na mchezaji mmoja mmoja kuwa na Messi, Mbappe na Neymar haitoshi unahitaji kuwa na watu zaidi ya timu.
Juventus kuna muda unashindwa kuwaelewa project yao nini ? Kibibi kizee cha Turin wakati wanafanya usajili wa Dusan Vlahovic , akiwa mfungaji anayeongoza kwa magoli kwenye ligi anashindwa kufunga kwa kukosa mtu anayeleta muungano kati yake na Dusan. CR7 akiwa Juventus wakicheza dhidi ya Ajax wakiwa na De Ligt, Ziyech na Tadic wanakufa 2-1 Turin unaona kabisa timu haichezi wote wanamuangalia CR7 unahitaji zaidi ya timu linapokuja suala la mashindano makubwa kama UEFA CL. Siku za usoni uwekezaji wao utawalipa kama watafanya mbadala wa Bonucci,Chiellini, Sandro, Dybala anahitaji changamoto mpya, Cuadrado pia si mbaya akapewa mkono wa kwa heri. Nakuruhu damu kama Demiral , Chiesa, Dusan na kina Locatteli nakuongeza sura mpya za wapamabanaji kama kina Scamacca.