Huu ni upuuzi kwa kiasi fulani hasa kwangu mimi..
Wote wanaotenda mambo kama hya, ama kujiua wenyewe kisa mapenzi ama kufeli mitihani na mfanano wa hayo, kwanza akilini mwao wanakuwa na jibu la aina moja, kama ni mtihani basi ye anakuwa anaamin katika kufaulu 100% hafikirii kama kuna lolote linatokea
So hapo jamaa yangu ye aliweka imani kwa mwanamke 100% kitu ambacho si sahihi unamuamin vipi binadamu mwenzio kwa 100%.. hata mama zetu kuna kipindi wanatuongopea(japo kwa lengo zuri) ile kunuwa eeh, kunywa baba, dawa tamu ee.. ila ukiyanywa ni machungu, sas ndio iweje ukamuamin mtu baki asiejua hata uchungu wako..
Narudia tena, ukimsomesha mwanamke moyoni amini upo unamsaidia mtu baki tu, suala la mapenzi ni uamuzi wake na muda wowote yaweza kubinuka tikitaka..
Sasa ona anaenda kuozea jela, ndoto zake, mipango yake na habar zake zote zimekomea hapo.. inatia uchungu saana.