Licha ya Manchester United kuongoza kwa magoli 3-0 hadi dakika ya 70 dhidi ya Timu ya Coventry City inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (Championship) lakini hadi dakika ya 90 zinakamilika matokeo yalikuwa sare ya magoli 3-3.
Baada ya kuongeza dakika 30 za nyongeza katika Nusu Fainali hiyo ya Kombe la FA, hakukuwa na mshindi ndipo mchezo ukaamuliwa kwa matuta na Man United kushinda kwa penati 4-2.
Hivyo, mchezo wa fainali utapigwa Mei 25, 2024 ukizikutanisha Manchester City dhidi ya Man United kwenye Uwanja wa Wembley Jijini London, England