Habari za wakati huu wakuu,
Kwa siku za karibuni kumekuwa na wimbi la mastaa kufunguliwa kesi za ubakaji au za unyanyasaji wa kijinsia kutoka kwa wenza wao, sasa unaambia hali sio shwari pale Old Trafford baada ya mchezaji wao mason Greenwood kufunguliwa kesi ya unyanyasaji wa kijinsia kutoka kwa mpenzi wake na kupelekea kukaa ndani kwa muda kabla ya kupewa dhamana.
Kitendo cha Manchester United kumtenga na kumuondoa Greenwood kwenye kikosi hicho kabla hata hukumu haijatoka ili kujua kwamba ana hatia au hana baadhi ya mastaa hawakubaliani nacho na wanaona kama ni usaliti kwa mwenzao kwani hukumu bado haijatoka katika kipindi hichi walitakiwa wawe naye pamoja na wampe ushirikiano kuliko kipindi chote cha maisha yao wakiwa old Trafford ila hali imekuwa tofauti kwao.
Tangu afunguliwe kesi baadhi ya wachezaji wenzake wamekata mawasiliano nae ikiwemo kujiondoa katika mitandao ya kijamii (unfollow) wakati huo club ya Manchester United wakitoa ofa ya kubadilisha jezi yake buree na kupewa jezi nyingine unayoitaka kumbuka yote yanafanyika ila hukumu haijatoka bado.
Baadhi ya mastaa wakiongozwa na Jese Lingard hawapendezwi na hali hiyo kwani hukumu bado haijatoka na kujua kama ana hatia au laa na kuifanya timu iwe na makundi mawili hasa ule upande wa wachezaji wenzake anaocheza nao timu ya taifa wanahisi anachofanyiwa muingereza mwenzao sio sahii kwani hukumu bado haijatoka na hastahili yote hayo.
Kumbuka mchezaji wa Manchester city BENJAMIN MENDY na yeye anakabiliwa na mashtaka kama hayo yakiwa yamefikia tisa kwa sasa ila club yake haija chukua uamuzi kama wa Manchester United kwani bado hukumu haijatoka na wanampa ushirikiano japokuwa wamesitisha mkataba mpaka hukumu itakapo toka ila sio kupiga marufuku jezi yake na kumondoa kwenye social media.
Kwa hali ilivyo kwa sasa man United mmoja lazima akubali matokeo ambao ni upande wa C.RONALDO au Jesse lingard ambapo kwenye mchezo uliopita aliomba asipangwe licha ya kukanusha ila nikusimamia msimamo juu ya rafiki yake au kocha wa muda mmoja wapo lazima akubali yaishe ila kwa sakata hili linahitaji mda pale man United ili iweze kurudi kama zamani na kupata matokeo mazuri.
N:B Rafiki wa kweli ni wazazi wetu wengine wote ni wanafiki tu hivyo tusijisahau,
Pole mason Greenwood hukustahili haya yote.