Man Utd atakufa 3-0 Stamford Bridge

Man Utd atakufa 3-0 Stamford Bridge

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Yale matatizo sugu ya Man Utd kesho jumamosi yatarudi upya wakati Chelsea itakapoialika Man Utd katika uwanja wake wa Stamford Bridge.

Ikumbukwe kocha Jose Mourinho wa Man Utd amekalia kuti kavu, na kesho anaenda kukutana na timu yake ya zamani iliyo katika fomu ya hatari.

Nani wa kuzuia movement za Jorginho pale kati? Wanasema Jorginho ni sigara ya pili ya Kocha Mauricio Sarri. Jorginho ndio anafanya timu nzima ya Chelsea inatiki.

Eden Hazard atazuiwa na nani? Utamu mwingine wa mechi hii utakuwa hapo. Kumtazama Hazard akiwa anacheza ni sawa na kumchungulia Beyonce akiwa anaoga, inafurahisha.

Kitu pekee Man Utd watajivunia kesho ni kupaki karandinga, sio basi tena. Kesho formation ya Man Utd itakuwa 7-3-0
Jose Mourinho hajawahi kupata walau saee anapotembelea Stamford Bridge. Hivyo anaelewa vyema ugumu wa mechi hiyo.

Kila la heri, The Blues, Keeping The Blue Flag Flying High. Tukutane kwanzia saa 8:30 kwa saa za Afrika Mashariki.
 
hata kama wachezaji wapo ktk mgomo huwa hawahujumu mechi muhimu kama hizo ambazo wanajua kabisa ndipo wanapouzia majina yao
 
Si kweli kwamba Mourinho hajawahi kupata hata sare darajani, alishakuja na inter na anashinda moja bila
 
Man United kufungwa Leo siyo habari na haitoshangaza mtu,Ila Chelsea kufungwa na united ni habari na itashangaza watu....Kwahyo kwa dhumuni la Uzi wako sioni kama kuna cha ajabu hapo
 
Back
Top Bottom