Man Utd Haikuwa Na Haja Ya Kumsajili Bruno

Cytochrome p450

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2019
Posts
5,638
Reaction score
15,044
Kwenye pita pita zangu leo mitandaoni nilifanikiwa kuingia kwenye page ya Sky Sport ya Instagram, Source ya michezo ambayo naiamini kuliko zote. Achana na hao wakina Shafii Dauda, maana kwenye page zao wamejaza ushabiki.

Kuna taarifa ya usajili nimeiona inayowahusu Man Utd kukaribia kufanya uhamisho wa mchezaji wa Sporting Lisbon, Bruno Fernandez.

Kwa upande wangu huu usajili naona hauna tija kabisa kwa Man Utd. Nilikuwa naamini hivyo tangu mara ya kwanza wahusishwe na kiungo huyo.

Ninachokijua kuhusu Bruno, kwamba ni kiungo mmoja wa kawaida sana. Amejaaliwa skills ndogo ndogo za kuchezea mpira lakini sidhani kama ndio sababu ya kumfanya aweze kufanya vizuri kwenye soka la uingereza. Kwangu mimi sioni tofauti aliyonayo yeye na Fred. Tena inawezekana Fred akawa ni mzuri zaidi kuliko Bruno.

Hatujui lakini mwisho wa siku itakuwaje, kila mtu na kismati chake.

By the way, we all wish him lucky!!
 
Aisee kwa hiyo bora kubaki na Lord Lingard kuliko Kuwa na Bruno? Mkuu fikiria tena ulichoandika.
Man united inataabika kila kukicha yote ni kukosa kiungo mbunifu pale mbele. Waliokuwepo wameshindwa kuonyesha kitu (Lingadinho, Mata & Pereira) Bruno ni chaguo sahihi kwa Man united.

GGMU
 
mtoa post jaribu kupunguza chuki binafsi kwa watu wengine kama shaffih Dauda lakin pia wewe usijifanye unamjua sana Bruno Fernandes na kumbeza juu ya uwezo wake unakosea sana mana inaonekana haujawai kumuangalia akiwa anacheza kwenye klabu na taifa lake.punguza mihemuko ya kiwaki
 
Sasa wewe unafikiri nani asiyemjua Shafii Dauda kama ana ushabiki kwenye uchambuzi wake?

Halafu, mimi siwezi kukurupuka tu kutoka usingizini kuandika mambo nisiyoyajua.

Haya niambie wewe, maajabu gani aliyoyafanya Bruno kwa timu yake ya taifa ya Ureno!
 
Yaani wewe wajifanya wamjua sana mchezaji kuliko wanaotoa bilioni zaidi ya mia? Wabongo acheni hizo.
 
Kwenye pita pita zangu leo mitandaoni nilifanikiwa kuingia kwenye page ya Sky Sport ya Instagram, Source ya michezo ambayo naiamini kuliko zote. Achana na hao wakina Shafii Dauda, maana kwenye page zao wamejaza ushabiki.

Kuna taarifa ya usajili nimeiona inayowahusu Man Utd kukaribia kufanya uhamisho wa mchezaji wa Sporting Lisbon, Bruno Fernandez.

Kwa upande wangu huu usajili naona hauna tija kabisa kwa Man Utd. Nilikuwa naamini hivyo tangu mara ya kwanza wahusishwe na kiungo huyo.

Ninachokijua kuhusu Bruno, kwamba ni kiungo mmoja wa kawaida sana. Amejaaliwa skills ndogo ndogo za kuchezea mpira lakini sidhani kama ndio sababu ya kumfanya aweze kufanya vizuri kwenye soka la uingereza. Kwangu mimi sioni tofauti aliyonayo yeye na Fred. Tena inawezekana Fred akawa ni mzuri zaidi kuliko Bruno.

Hatujui lakini mwisho wa siku itakuwaje, kila mtu na kismati chake.

By the way, we all wish him lucky!!
Watanzania nyinyi ndio makocha ,mascout,ma sport directors ,ma pundicts ,ma fans ,ma sports analysistics ,ma much know hongera mkuu umeangukia kwenye hili group .
 
Mtoa mada utakuwa una corona ya kufikiri wewe na usirudie kabisa kumsema vibaya bruno tutakuhamisha hata hapa
 
Back
Top Bottom