Wahenga walipata kusema kuwa KAMWE HAUWEZI KULA MUWA BILA YA KUKUTA FUNDO....maana yake ni kuwa matatizo ni sehemu ya maisha na njia pekee ni kupambana nayo na sio kuyakimbia....
Lazima tutambue kuwa maisha ni safari ndefu sana....na sio kila muda katika maisha mambo yatakuwa jinsi ambavyo sisi tunataka yawe......sio kila wakati tutapata matokeo mazuri ya kile ambacho tumekikusudia la hasha....lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya sisi kuvunjika moyo na hata kujidhuru......
Kwani pamoja na hayo magumu tunayopitia bado muumba ametujaalia uhai na afya kama nafasi ya kujaribu tena na sio kujitoa uhai......
Kujitoa uhai ni kuidhurumu nafsi yako.....kwa kuwa wengi wapo kama wewe lakini wamechagua kupambana na hali zao......
Hata wale unaowaona barabarani wakiwa na nyuso za furaha si kwa kuwa mambo yao ni mazuri la hasa bali wameamua kupambana na hali zao.....