TRIPLE H
JF-Expert Member
- Feb 18, 2013
- 651
- 349
Amani iwe kwenu wakuu,
Nimekuwa nafuatilia 'manabii wa kisasa' na kulinganisha na kile kinachofanywa na waganga wa kienyeji nikaona kama vile kuna mfanano wa namna fulani kiasi kama wangekuwa hawatumii majina tofauti ingekuwa vigumu sana kuwatofautisha.
Kwa mfano; unakuta nabii anakutokea na kuanza kukuambia mambo ya siri ya maisha yako kama vile anayekuloga, mume uliyetembea naye, mchepuko wako, mtoto uliyezaa kwa mume mwingine na ukaficha na kadhalika nakadhalika. Mambo kama hayo yamekuwa yakisemwa na waganga wa kienyeji vile vile.
Sasa naomba kuuliza mnisaidie jamani:
1. Watu hawa chanzo cha wao kujua siri zetu ni nini?
2. Je, wana vyanzo tofauti vya habari zao au mafunuo/maono yao?
3. Kuna faida gani za 'nabii wa kisasa' kutabiri mambo mepesi-mepesi kama hayo ambayo tangu zamani tunajua waganga ndio wamekuwa wakiyabashiri?
Naomba kuwasilisha.
Ahsanteni...
CC: Mshana jnr
Zitto jnr