MGILEADI
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 1,621
- 1,545
Mkuu MGILEADI,
Nimekusoma vizuri lakini ulichofanya ni kunukuu maandiko yanayotofautisha manabii (wa Kristo na wa uongo)
Nilichotaka kujua si tofauti ya manabii, bali tofauti ya unabii 'wa kisasa/kizazi hiki' na uganga wa kienyeji!
Kuna tofauti gani hasa?
Manabii wa leo ambao wanatumia vifaa (mafuta, maji, chumvi) zaidi badala ya Jina la Yesu ni rahisi kufananishwa na waganga wa kienyeji. Nabii ambaye anafanya utambuzi pia huwezi kumtofautisha na waganga. Matumizi ya vifaa yanafanana na hirizi za mganga. Kupenda malipo ya fedha kwa huduma inayotolewa pia ni kielelezo cha tabia waliyo nayo waganga maana kwao ile ni kazi. Manabii wengine wanauza yale maji na yale mafuta. Hii si sawa. Ukilaani maadui zako kadhalika ni tabia ya waganga na haipaswi kwa nabii halisi wa Mungu. Kumweleza mshirika kuwa huyu si mkeo ama mumeoama wanavyofanya manabii wengine ni tabia za waganga wengine kwa ramli zao chonganishi. Kutabiri mabaya kama vile ndege itaanguka baharini, timu ya taifa itafungwa na ushindwa mechi ni mambo ya wasihiri na siyo yanayomhusu Nabii wa Mungu sawasawa. Ukipandisha mapepo na kuanza kuongea nayo kwa muda mrefu ni kama unawabembeleza. Manabii wa Mungu hawapaswi kuyapunga mashetani bali kuyafukuza na wasiwape nafasi kusema kitu. Nitaendelea.