Manabii wa uongo

Manabii wa uongo

koncho77

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
7,789
Reaction score
10,388
Jamaa mmoja akiwa na mtutu wa kivita maarufu kama AK47 alivamia kanisa moja la kiroho na kukuta watu wanafanya ibada. Akiwa ameuelekeza mtutu wake juu jamaa alianza kupaza sauti huku akielekea madhabahuni. “Nani ni mtoto wa mungu hapa?” Jamaa alihoji kwa ubabe. “Nauliza hivi, nani ni mtoto wa mungu hapa ili nimpeleke sasa hivi kwa baba yake mbinguni!”

Waumini wote walikaa kimya na jamaa akaongeza mkwara kwa kufyatua risasi tatu kwenye paa la kanisa. Waumini wote
wakapaza sauti, “ni mchungaji. Kila siku huwa anasema yeye ni mtoto wa mungu.”

Kwa upole na unyenyekevu mwingi mchungaji akajibu, “mbona mnanisaliti wapendwa? Nyote nyie mnajua kwamba mimi ni mtoto wa Githinji. Sasa ninahusianaje na huyo mungu.
 
Hahaha, kama yule mama aliyesema anampenda sana mumewe na mumewe alipofariki mama akaambiwa atumbukie kaburini azikwe na mumewe kwa sababu anampenda. Mama alichana mbuga akapotea.Hahahaha.
 
Hahaha, kama yule mama aliyesema anampenda sana mumewe na mumewe alipofariki mama akaambiwa atumbukie kaburini azikwe na mumewe kwa sababu anampenda. Mama alichana mbuga akapotea.Hahahaha.
Chezea kufa
 
Dhana ya woga ipo kwa viumbe vyote, usiegemeze kipimo chako kwny dini tu.
Hata ww waweza isaliti familia yako mbele ya mtutu.
 
Dhana ya woga ipo kwa viumbe vyote, usiegemeze kipimo chako kwny dini tu.
Hata ww waweza isaliti familia yako mbele ya mtutu.
Haitatokea na haiwezi kutokea hata siku moja nikaisaliti familia yangu.
Utakuwa ni ujinga ulioje huo
 
Back
Top Bottom