Kama umemjulia Manara akiwa Simba bado humjui Manara, huyo ni tatizo tangu akiwa Ccm, majukwaa aliyekuwa akipanda Manara ni matusi kwa CUF na watu wa Ccm wakamjaza kichwa kwamba ndio kiboko ya CUF.
Manara ameharibika tangu akiwa Ccm haya unayoyaona leo ni madogo.
Pamoja na mema yote aliyofanya GSM kwa Yanga, lakini kitendo cha kumleta Manara Yanga ametukosea sana tena sana.
Anachokifanya Manara sasa si kwamba ana mapenzi na Yanga, Bali kisasi chake binafsi na Simba.
Nashangaa sana taasisi kubwa kama Yanga inakaa kimya kuchonganishwa na Simba wakati Yanga haina ugomvi wowote na Simba.
Manara hayupo kwenye utani wa jadi, Manara anatumia platform ya Yanga kutowa nyongo zake kwa Simba hili halikubaliki.
Na kwa watu wenye akili timamu ni kweli Manara alikuwa akiwahujumu Simba na Madam Barbara alikuwa Sahihi sana.
Muda huwa ndio unaamuwa kila kitu, kama kuna mtu wa Yanga mpaka leo haoni tatizo kwa Manara basi atafute mchezo mwingine wa kushabikia kwenye football hakumfai maana atakuwa hajui lolote kuhusu mpira.
Manara akae hukohuko GSM, ila Yanga hatumtaki kabisa.