Haji Manara amesema soka ni mchezo muhimu sana, inaweza simamisha vita, kuleta vita na hata kuwaleta watu pamoja au kubaguana. Amesema kiongozi mmoja mkubwa serikalini alimpigia simu na kumwambia aendelee kuongelea soka na kuchamba watu ili watu wasiendelee kuhoji kupanda kwa bei ya mafuta na mfumuko wa bei. Je sisi wananchi huwa tunatambua haya sana sana tunapokuwa tunadai vitu vya msingi?