Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona waandishi kibao tu wana diplomaKumbe ni kosa mwandishi kuwa na diploma?
Watangazaji wa mpira uwezi wao mudogo badala ya kutangaza mpira wanakuwa busy na vitu vingine unaambulia kusikia gooooo!Haji Manara amekuwa Mtanzania wa kwanza kuongea mbele ya umma na kuonyesha kutofurahishwa na suala la Wachambuzi wa michezo kupewa mafunzo na kusomea fani hiyo.
Ameandika Manara kwenye ukurasa wake wa Instagram,
"Hivi hii nchi tumerogwa na nani? Yaani tuache kushughulikia Vipaumbele vya maana kama kukarabati Viwanja vyetu vibovu, kutengeneza Viwanja vya mazoezi, kutengeneza misingi ya Watoto wetu na kusaka vipaji, tunataka kupeleka pesa kwa ajili ya mafunzo eti kwa 'Wachambuzi'.
Nchi gani duniani mshawahi kusikia inawekeza pesa zake kusomesha Wachambuzi wa football au michezo mingine? İli iwe nini ? Uchambuzi ni karama na mafunzo yoyote ya ziada ya kimaadili au ya kiweledi hutolewa na Media husika kwa jinsi wanavyotaka Wachambuzi wao wakaongee nini !!
Ni matumizi mabaya ya pesa na kupoteza muda tu kwa kutaka kuwapa mafunzo watu ambao sio kipaumbele chetu kwa sasa, tumeshindwa kupeleka hata Refa mmoja AFCON , leo tukatoe pesa za Walipa kodi kusomesha Wachambuzi, Why tusitoe mafunzo sahihi kwa Waamuzi wetu?
Hatuzalishi Makocha wa maana kama Nchi na hatuna hata Kocha mmoja anaefundisha Soka nje ya mipaka yetu, tunashindwa hata na Burundi tu, badala ya kuwekeza huko tunahangaika na kundi ambalo halina athari katika maendeleo ya mpira wetu kwa ukubwa huo.
Shida kubwa tuliyonayo hatujui nini tunataka kama Nchi, hatujui tumekwama wapi na nini tufanye ili kupata maendeleo waliyonayo wenzetu katika football, leo tunataka Chuo chetu cha Michezo kitumie Rasimali zake kusomesha Wachambuzi, kesho si ajabu mkapeleka Boll Boys wakafundishwe mbinu sahihi za kuokota mipira, tupo serious kweli na football?
Wadau haipo nchi duniani inasomesha Wachambuzi wake sana sana ni Media husika zenyewe kwa kuwapa mafunzo ya mwelekeo wa chombo husika, Serikali yetu katika hili, pamoja na Ukada wangu kwa Chama Changu kinachoongoza Serikali yetu, Siungi mkono mpango huu na nauona hauna maaana kwetu kama Taifa, Najua nyie ni Wasikivu na mtaachana na mambo yasio na faida kwa Nchi, hangaikeni kutengeneza football Academy ya maana moja japo kwa kuanzia, wapeni mafunzo ya ziada Waamuzi na Makocha na hata Viongozi wanaoongoza mpira,andaeni mafunzo sahihi ya Management Skills,,,Wachambuzi tuziachie Media husika zitawaelekeza nini waseme na nini wasiseme ,,
Sorry kama nimewakwaza lakini hyo ni fact no matter what!!"- Haji Manara
Nini maoni yako?
Written by Mjanja M1 [emoji3578]
Unataka akuoe wewe?, Acha kujadili maisha ya mtu. Jadili hoja yake.na yeye achane kuoa mademu za watu
Ameongea kitu sahihi ila sababu zilizomfanya afungiwe sio hiziAmesema kweli ..
Hii ndiyo sababu kama hizi zilimfanya afungiwe.
Kuwa mkweli sana
Kama watu wanasomea michezo, kwa nini wasisomee uchambuzi wa michezo au mchezo. Uchambuzi siyo kitu anaweza kila mtu. Hata wanaoweza wanatakiwa kunolewa, ili waangalie vigezo vya kuchambulia. Nchi nyingi wachambuzi wa michezo huwa ni wachezaji wastaafu katika mchezo. Hata hao wanamichezo wastaafu hupata semina za uchambuzi. Kwa hiyo siyo mbaya wachambuzi kusomea fani hiyo. Kwani kusomea maana yake nini? siyo lazima iwe cheti, diploma, au digrii. Naona kama watu wanadharau michezo. Michezo ni fani (profession) na ajira. Kwa hiyo wahusika na michezo wanahitaji kuwa na taaluma ya michezo, kusema kuwa watu hawahitaji kusomea ni kuidharau michezo. Kwani Manara anaogopa nini kuona watu wanasomea michezo. Basi tufute taaluma nzima ya michezo, kama hatutaki watu muhimu kama wachambuzi nwasomee na kuwa na uelewa wanapochambua wanatumia vigezo, au tunataka wachambuzi vilaza kama yeye.He is right naunga mkono hoja
Manara hapingi wachambuzi kusomea hiyo taalama, anapinga Kodi ya Watanzania kutumika kwa shughuli hiyo badala ya kutumika kwenye vipaumbele alivyo vitaja yeye.Kama watu wanasomea michezo, kwa nini wasisomee uchambuzi wa michezo au mchezo. Uchambuzi siyo kitu anaweza kila mtu. Hata wanaoweza wanatakiwa kunolewa, ili waangalie vigezo vya kuchambulia. Nchi nyingi wachambuzi wa michezo huwa ni wachezaji wastaafu katika mchezo. Hata hao wanamichezo wastaafu hupata semina za uchambuzi. Kwa hiyo siyo mbaya wachambuzi kusomea fani hiyo. Kwani kusomea maana yake nini? siyo lazima iwe cheti, diploma, au digrii. Naona kama watu wanadharau michezo. Michezo ni fani (profession) na ajira. Kwa hiyo wahusika na michezo wanahitaji kuwa na taaluma ya michezo, kusema kuwa watu hawahitaji kusomea ni kuidharau michezo. Kwani Manara anaogopa nini kuona watu wanasomea michezo. Basi tufute taaluma nzima ya michezo, kama hatutaki watu muhimu kama wachambuzi nwasomee na kuwa na uelewa wanapochambua wanatumia vigezo, au tunataka wachambuzi vilaza kama yeye.