Manara apinga Wachambuzi kupewa Mafunzo

unajichekesha nini tuna kusagia kunguni mpaka urudi kuimba nyimbo zako pesa sio matako
 
Hili la kusomea uchambuzi Mwana FA aliingizwa chaka itakua ni Karia ndo alimuingiza Chaka ili baadae kuwe na mpango wa kuwadhibiti
 
Watangazaji wa mpira uwezi wao mudogo badala ya kutangaza mpira wanakuwa busy na vitu vingine unaambulia kusikia gooooo!
 
He is right naunga mkono hoja
Kama watu wanasomea michezo, kwa nini wasisomee uchambuzi wa michezo au mchezo. Uchambuzi siyo kitu anaweza kila mtu. Hata wanaoweza wanatakiwa kunolewa, ili waangalie vigezo vya kuchambulia. Nchi nyingi wachambuzi wa michezo huwa ni wachezaji wastaafu katika mchezo. Hata hao wanamichezo wastaafu hupata semina za uchambuzi. Kwa hiyo siyo mbaya wachambuzi kusomea fani hiyo. Kwani kusomea maana yake nini? siyo lazima iwe cheti, diploma, au digrii. Naona kama watu wanadharau michezo. Michezo ni fani (profession) na ajira. Kwa hiyo wahusika na michezo wanahitaji kuwa na taaluma ya michezo, kusema kuwa watu hawahitaji kusomea ni kuidharau michezo. Kwani Manara anaogopa nini kuona watu wanasomea michezo. Basi tufute taaluma nzima ya michezo, kama hatutaki watu muhimu kama wachambuzi nwasomee na kuwa na uelewa wanapochambua wanatumia vigezo, au tunataka wachambuzi vilaza kama yeye.
 
Manara hapingi wachambuzi kusomea hiyo taalama, anapinga Kodi ya Watanzania kutumika kwa shughuli hiyo badala ya kutumika kwenye vipaumbele alivyo vitaja yeye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…