Manara asema ataishitaki Simba

Manara asema ataishitaki Simba

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
Aliye kuwa msemaji wa Simba na sasa msemaji wa Yanga Haji S Manara amesema ataishitaki Klabu ya Simba kwa kumtumikisha bila mkataba.

Manara ameyasema hayo akiwa anafanyiwa mahojiano na Divathebawse kwenye kipindi cha lovedavi cha Wasafi FM. Manara amesema Klabu ya simba ilimtumikisha kwa zaidi ya miaka 6 pasipo kuwa na mkataba hivyo ataishitaki club hiyo.

Manara ameongeza kwa kusema ataishitaki club hiyo baada ya kutoka kwenye mechi zake za club bingwa, pia amesema yeye ndiye alie fanya Simba ifahamike kwa kuwavuta mashabiki wengi kushabikia Simba.

Pia Manara amesema ndani ya simba kuna watu wanao mpa taarifa ya yanayo jilisababu kuna watu wanamfuatilia Manara.

Ameendelea kwa kusema simba imemuhujumu sana hadi kuingilia baadhi ya biashara zake za ubalozi wa makampuni, pia amesema ana siri nyingi za simba ambazo hata robo hajawahi kuzisema hivyo ipo siku siri hizo atazitoa hivyo ikifika muda huo siri zote atazitoa labda wamuuwe lakini kama yupo hai atazisema.
 
Huyu jamaa baada kutoka SIMBA amekuwa galasa tu na mpk umaarufu wake umeshuka
sasa anatafuta namna ya kuboost ndo kaona aje na hicho kiroja.

katika dunia mambo hayaji mara mbili ikitokea ni one time sasa ukaja ukazingua hiyo chansi
basi we sahau fanya mambo mengine

Namshauri kwa hizo senti chache anazopata kwa sasa ajaribu kuwekeza kwenye biashara yoyote ili asije kuadhirika baadaye
mana huko mbele ninaona dhahili anaenda kupoteza kabisa hata ile thamani ndogo alokuwa nayo sasa
hvyo awe makini na dunia hii siyo awe lelemama yeye mwanaume shauri yake
 
Ukitaka kuyajua maumivu ya mwanamke alieachwa na mume ambae bado anampenda Basi muangalie manara ni mfano mzuri wa mwanamke alie achika huku bado anahitaji ndoa.

Yan atakuja kudai had vijiko aseme mlitafuta wote ilimrad tu akukomoe na akiona hukomoleki yuko tayari akutangaze ulikua kibamia hata kma ulikua unamkuna had anaomba break au anaweza akuloge
 
Ukitaka kuyajua maumivu ya mwanamke alieachwa na mume ambae bado anampenda Basi muangalie manara ni mfano mzuri wa mwanamke alie achika huku bado anahitaji ndoa...
Kweli kabisa huyu jamaa anashangaza
 
Aliye kuwa msemaji wa Simba na sasa msemaji wa Yanga Haji S Manara amesema ataishitaki Klabu ya Simba kwa kumtumikisha bila mkataba...

Mimi sio Simba wala Yanga,wala sio shabiki wa Mpira wa miguu ila kwa haya anayofanya Haji ni kama anatafuta watu wamdhalilishe kwa nguvu.

Anatishia kutoa siri za watu wakati yeye mwenyewe anajijua alivyo mchafu,watu wakianza kusema yake sijui uso wake ataweka wapi!!.

Kama anahisi anawajua sana watu na siri zao,basi ajue na yeye yake watu wanayajua vizuri.

Watu wanasemaga “msenge” hana mkole kumbe ni kweli!
 
Manara ni msemaji wa Yanga lakini anaisema Simba badala ya kufanya kilichomlpeleka yanga

Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
Kabisa. Kuacha au kuhama kazi ni jambo la kawaida na huna sababu ya kuendelea kuiandama sehemu uliyohama. Anatakiwa ajipange aangalie mbele mambo gani ya ubunifu atayafanya kwa muajiri wa sasa.
 
Hakuna hata mmoja aliyezungumzia hayo madai yake ya kufanyishwa kazi bila mkataba miaka 6 zaidi ya kumlaumu hapo napo kuna tatizo.
 
Back
Top Bottom