Manara ateuliwa tena kuwa Msemaji Rasmi wa Klabu ya Simba

Manara ateuliwa tena kuwa Msemaji Rasmi wa Klabu ya Simba

Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba imemteua Haji Manara kuwa msemaji rasmi wa klabu hiyo.

"Asanteni Sana Wanasimba wote hususan Bodi ya Wakurugenzi chini ya Mwenyekiti wetu Mohammed Dewji,lakini kubwa kwa CEO wetu mpya Mr Senzo kwa kuendelea kuniamini kufanya kazi katika Klabu hii kama Msemaji wao rasmi, Insha'Allah ntaendelea kufanya kazi hapa kwa spirit ile ile” ameandika Haji Manara mtandaoni.
Alafu wengine tunaanza kusahau kiswahili..Manara atoage na madongo ya kizungu tuelewe wote.
 
Hapo sawa.

Kwahiyo msemaji ni mtu asiye na taaluma yeyote, kazi yake ni kuongeangea utumbo tu.

Mfano
"Mikia hii hata Man City au Barca wakija tutawafunga tu",

"Kikosi chetu ni cha bilioni 3".

"Mbumbumvu hii tusipofika robo fainali ya Club bingwa Africa Mnitupe mtoni niliwe na Mamba"
Ikiuma chomoa..., ni wazi hapa umejijaza upepo kidude kikachomoka.
 
Waliotaka afutwe kabisa nawaona tu wanavyojichubua.

Mnyama nguvu moja
 
Kuna kipindi alikua anajiita mkuu yaani head wa kitengo cha habari ndani ya simba sport club....leo amekua msemaji???
 
Vyura mnapokezana verse...... wana msimbazi tunawacheck tu!
.Manara karudi kwenye nafasi yake!!
 
Ndo maana tunawaambia simba timu ya watu! na lengo letu ni kumshinda mshindani wetu ili mashabiki tuwe na furaha wakati wote. kama manara ni mwana yanga anakuja kuifurahisha simba na kuihudhunisha yanga kwetu sisi ni jambo jema sana......

Manara, kimwili yupo simba ila ki roho yupo yanga...
 
Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba imemteua Haji Manara kuwa msemaji rasmi wa klabu hiyo.

"Asanteni Sana Wanasimba wote hususan Bodi ya Wakurugenzi chini ya Mwenyekiti wetu Mohammed Dewji,lakini kubwa kwa CEO wetu mpya Mr Senzo kwa kuendelea kuniamini kufanya kazi katika Klabu hii kama Msemaji wao rasmi, Insha'Allah ntaendelea kufanya kazi hapa kwa spirit ile ile” ameandika Haji Manara mtandaoni.
Msemaji au Afisa Habari?
 
Back
Top Bottom