Pre GE2025Manara: Utani wa Simba na Yanga umesaidia kuleta Utulivu nchini, utakuta Maji, Sukari na Umeme hakuna lakini Media zinajadili Simba na Yanga!
Katibu Uenezi wa CCM mkoa wa DSM mstaafu Alhaj Hajji Manara amesema Utani wa Simba na Yanga umesaidia kuleta Utulivu nchini na Serikali inauunga mkono 100%
Manara amesema unaweza kukuta Maji hakuna, Umeme hakuna, Sukari hakuna lakini Wananchi kwenye mitandao ya Kijamii wako busy kuwajadili Pacome na Chama nani mkali
Manara amesema Utani wa Simba na Yanga umefanya Siasa za Tanzania kuwa nyepesi na rahisi sana
Credit: Mfanyakazi Online
Baadae Mlale Unono πππ₯
======
Your browser is not able to display this video.
Utani wa Simba na Yanga umesaidia kuleta utulivu katika Siasa za Tanzania na Serikali inauunga mkono kwa asilimia mia kwa sababu kuna wakati ajenda inakuwa Simba na Yanga lakini huku umeme hakuna, maji yamekatika huku sukari hamna lakini watu wanafocus na Pacome na Chama nani zaidi, umeme hakuna, maji hakuna, sukari iko juu lakini ajenda kwenye Social media watu Pacome na Chama nani zaidi.
tangu nianze kumsikiliza manara leo ndo kaongea jambo la kutafakari sana.........kwamba ushabiki wa simba na Yanga una manifaa kwa nchi yetu au ni hatari unaua vijana wengi.
Ofcoz Simba na Yanga zinatumuka. Ndio maana leo stori ya Magoma na Yanga imetengenezwa ili kufanya diversion ya stori ya Nape anavyotuibiaga kura.
Na kwasababu watanzania hawajui kinachoendelea huku duniani, kila kitu kwao poa tu na ndo maana Nape sio mara ya kwanza wala ya mwisho kutuambia hivyo kwasababu anajua hata atuambie nini, hatuwezi mfanya chochote. Safi sana Nape
Mpaka uwe na Akili kubwa ndiyo utajua kauli hii ya manara... Angalia Leo watanzania wote wamehamishwa kutoka Kwa NAPE Hadi YANGA.
Nchi hii ni UJINGA mtupu watu wanajadili kutoka asubuhi vipindi vyote redioni ni michezo,udaku na michezo tena usiku. CCM wamafanikiwa pakubwa Sana kuwaingiza watu wake kwenye UJINGA
Hii video inaeleza/fafanua mambo mengi sana yanayotrend..
NB zingatia na hukumu ya kina mzee magoma tangu august 2023 na kukamata trend sasa hivi.[URL
Your browser is not able to display this video.
======
Utani wa Simba na Yanga umesaidia kuleta utulivu katika Siasa za Tanzania na Serikali inauunga mkono kwa asilimia mia kwa sababu kuna wakati ajenda inakuwa Simba na Yanga lakini huku umeme hakuna, maji yamekatika huku sukari hamna lakini watu wanafocus na Pacome na Chama nani zaidi, umeme hakuna, maji hakuna, sukari iko juu lakini ajenda kwenye Social media watu Pacome na Chama nani zaidi.
Siasa ni trust, hakuna hao wanasiasa wenye nguvu hiyo ya ushawishi Tanzania (demagogue politics, Magufuli kidogo ndio alifanya watu kuwa interested).
Ndio maana wananchi hawajali sio kwamba wanafurahia shida. Akitokea mtu wa kuaamsha wataamka tu.
Vinginevyo jaribu kutafuta sports radio za wazungu usikilize povu la team zao siku ikifungwa, kuna mashabiki wanasafiri na team msimu mzima.
Ushabiki wa mpira uingereza ni kama dini ndio maana makocha hawadumu; na siasa ina nafasi vilevile. Wanasiasa waache kulaumu raia ambao hawajui haki zao kwa kushindwa kazi kuelemisha jamii.
Katibu Uenezi wa CCM mkoa wa DSM mstaafu Alhaj Hajji Manara amesema Utani wa Simba na Yanga umesaidia kuleta Utulivu nchini na Serikali inauunga mkono 100%
Manara amesema unaweza kukuta Maji hakuna, Umeme hakuna, Sukari hakuna lakini Wananchi kwenye mitandao ya Kijamii wako busy kuwajadili Pacome na Chama nani mkali
Manara amesema Utani wa Simba na Yanga umefanya Siasa za Tanzania kuwa nyepesi na rahisi sana
Inasikitisha na kushangaza sana. Miaka zaidi ya 60 ya Uhuru,nchi ambayo inasemekana tuna utajiri wa maji kuliko nchi yoyote ukanda huu wa maziwa makuu na pengine Afirka nzima,leo tunajadili swala la mgao wa maji.Tena Kuna wengine wameenda mbali zaidi kwa kuandika makala za kuwasifia Waislamu...