DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Wakili Mwandamizi wa Serikali na mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM Bw. Manchare Suguta Heche, leo Jumanne Julai Mosi 2025, amechukua fomu ya kukiomba chama chake, Chama Cha Mapinduzi CCM, kumpatia ridhaa ya kuwania Ubunge kwenye Jimbo la Tarime Mjini katika Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu.
Wakili Heche mara baada ya kuchukua fomu hiyo, amezungumza na wanahabari kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Tarime Mkoani Mara akibainisha kuwa lengo la kuwania Ubunge katika Jimbo hilo ni kutokana na kuwa mzaliwa wa eneo hilo, akisema anazijua kikamilifu fursa na changamoto za Jimbo hilo na sasa yupo tayari kushirikiana na wananchi wa Tarime Mjini katika kujiletea maendeleo.
"Mtakumbuka Mwaka 2020 mimi pia nilishiriki, tulikuwa watu 27 na kwenye tano bora mimi nilikuwepo na Siasa ni sayansi kuna mambo ya kujifunza na kuboresha na safari hii nitawashangaza watu, nimedhamiria kuja hapa kushinda na sio kushiriki, naamini wajumbe wanatambua uwezo wangu, nimekuwepo serikalini kwa miaka 20 nikitumika kama Wakili mzoefu kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo Ofisi ya Makamu wa Rais na Chama kunitumia kwasasa hivi bado itakuwa ni muendelezo uleule, ni mtu ninayeweza kazi, ninayeweza kubuni na kuisimamia kazi kikamilifu" Amesema wakili Heche.
Heche kadhalika amebainisha kuwa yupo timamu katika kusimamia Ilani ya Uchaguzi ya Chama chake ya 2025/30, akiwasihi wananchi wa Tarime kumtuma kwenda kuwawakilisha, akieleza kuwa kwasasa anasubiri mchakato ndani ya chama kuweza kuendelea.