1. mkuu nimeshaongea sana humu Tecno haziuzwi bei rahisi, bei za Tecno ni sawa sawa na samsung na sometime samsung bei zake ni rahisi kuliko tecno. na ikumbukwe samsung kidunia si kampuni inayotengeneza bidhaa nzuri za bei ya chini hivyo mpaka kufikia stage simu za samsung kuwa sawa na tecno ina maana tecno nao wanauza bidhaa bei ghali.
angalia specs za simu hizi
-galaxy j7 prime (aggrey around laki 5)
-honor 5x huawei (kuna mtu amenambia laki 5 tigo)
hizo simu zinatoka kampuni kubwa duniani lakini zinauzwa bei rahisi kuliko phantom mpya hebu niconvice kuwa tecno wanauza bei rahisi
ukija makampuni ya kichina kama xiaomi, na le eco ndio kabisaa utaona unadhulumiwa kwani simu kama xiaomi redmi pro 3 ina specs kubwa kushinda tecno yoyote ile iliopata kutengenezwa toka kampuni ianzishwe lakini inauzwa dola 150 tu na maeneo kama kenya inauzwa laki 4 hivi, wanaship hadi Tanzania. ukija za bei rahisi xiaomi simu zao za bei rahisi ni around dola 75 hivi na zina specs kama hao kina c9 wanaouzwa zaidi ya laki 3. mfano kama hizi redmi mpya unaweza ziangalia hapa gsmarena
Xiaomi Redmi 3s - Full phone specifications
Xiaomi Redmi 4a - Full phone specifications
2.mediatek ni soc dhaifu hata kesho Apple akitumia mediatek tutaiponda huo ndio ukweli
-hazikai na charge
-virusi kila siku (tembelea jukwaa la tech malalamiko kibao),
-app inajipa root yenyewe (loop za toolkit)
-hazina custom rom za aosp
-update ni za kuunga unga na hazina monthly updates za ulinzi
-gpu dhaifu
-modem dhaifu
etc etc
kuna mambo mengi sana mediatek inapitwa na qualcomm, exynos na A series za apple.
3. nipe link hio ya iphone 6 na c9 tuone, sina c9 ila ninayo j8 ukitaka naweza kukuekea sample na simu kama s5 ambazo zote kwa sasa zinapatikana almost bei moja.
4. napinga simu za Tecno hazikai na chaji labda useme vile vitofali vyenye 5000mah kupanda na uzito unaozidi gram 200. kama mtu anaproof aeke hata screenshot ya battery na matumizi yake tuone.
swali la kizushi hili huwa nawauliza wadau wa Tecno miaka nenda miaka rudi ila hawanipi jibu
ni wapi tecno zimekaguliwa kuwa zinafaa kwa ajili ya matumizi ya binadamu?