El profesor
Member
- Jul 30, 2019
- 10
- 14
Mkoani Morogoro, kuna mji mdogo unaoitwa Matombo ambao maana yake ni matiti ya mwanamke.
Sababu ya mji huo kuitwa hivyo ni miamba ya mawe iliyopo eneo hilo, ambayo imeshikana kama matiti ya mwanamke.
Kwa Kiluguru matiti ya mwanamke huitwa matombo...na hiyo ndiyo asili ya eneo hilo kuitwa Matombo.
Na hii ndiyo asili pia ya mji wa Manchester nchini England, kuitwa jina hilo.
ILIVYOANZA
Jina la Manchester ni muunganiko wa maneno mawili, Man na Chester.
MAN
Neno hili ni la asili ya lugha ya Celtic, Mamm, lenye maana ya breast-shaped hill, yaani mlima wenye umbo la manyonyo (matiti).
.
CHESTER
.
Hili ni neno lililotoholewa kutoka neno la ceastre lenye asili ya kabila la Saxon ambalo maana yake ni ngome.
Wasaxon nao waliliiba neno hili kutoka neno la kilatini la 'castrum', ambalo ndiyo NGOME.
Warumi walipoitawala England, walijenga ngome katika maeneo mengi ya nchi hiyo, ikiwemo kwenye ule mji wa matiti wa Mamm.
Ngome hiyo ikaitwa Mamm-ceastre yaani ngome ya matiti (matombo)...jina hilo likabadilika badilika kutokana na nyakati, hadi kuwa Manchester kama lilivyo sasa.
.
.
ONGEZEA NA HII
Kama ilivyobainishwa hapo juu, Warumi walijenga ngome katika maeneo mengi...na ngome zote ziliishia na neno lile lile la Chester, kama iliyokuwa kwa Manchester.
Hapa utaukuta mji Colchester, inakotoka timu iliyoifunga Tottenham hapo jana kwenye Carabao Cup.
Kutokana na nyakati na matamshi, ngome zingine zikajikuta zinabadilika kidogo na kuishia na neno caster kama Doncaster inakotoka timu ya Doncaster Rovers, au cester kama Leicester inakotoka Leicester City.
Hiyo miji yote imetokana na zile zile ngome za ceastre zililillzoanza kama castrum.