Manchester united baba hajitambulishi, anaonesha matendo

Manchester united baba hajitambulishi, anaonesha matendo

Bacary Superior

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2014
Posts
3,721
Reaction score
1,514
Imeandaliwa na Bakari Ally
Simu: 0659-767121

Habari sana rafiki ni kipindi kirefu sana sijakuwa na
nyie katika upande wa kuandika makala lakini
nakuwa na muda mchache sana maana huu mwaka
ni KAZI TU, Ukifanya mzaha mkuu wa kaya
utajuana nae ila leo nakuja ni kisa kimoja hivi;
Mwishoni wa Miaka ya tisini (90) na mwanzoni wa
miaka ya elfu mbili (2000) wakati tunaishi Lindi huku
nikiwa na miaka kama 5 hivi tulikuwa tunapenda
sana kucheza kwa watoto wenzetu hapo tangu
tuliotoka mchana kurudi inakuwa jioni mida ya saa
kumi ili tuwai kufika nyumbani kabla ya Baba
hajarudi kutoka kazini kwake maana kama yeye
akianza kufika nyumbani kazi inakuwa kwetu kama
viboko au makofi ukisamehewa ujuwe unakuwa
kakufokea sana.
Akirudi Baba tu nyumba inakuwa tofauti watoto wote
tunatulia, hakuna kuongea ujinga wala ukitumwa na
mama hauwezi kukataa.
Kiukweli ivyo inavyotakiwa nyumba yoyote Baba
anatakiwa ajulikana kama yupo au hayupo na siku
zote BABA HAJITAMBULISHI maana ata akifika
mgeni lazima atamjua baba kuwa ni yupi wala
haulizi kuwa baba ni yupi katika hiyo nyumba.

Kama ukiona wewe hapo kwenu au unamuambia
mkeo/mwanao kuwa Unajua mimi mumeo/Baba
ako? Ujue kabisa umekosa vigezo siku zote Baba
wa Ukweli hajitambulishi utamjua tu, kitendo cha
kumuambia mkeo au mwanao kuwa wewe Baba
maana ake wewe haufanyi majukumu yako ya
Ubaba pole sana kwahilo...

Ila kuna wakati Baba kiukweli akuwa anaelekea
kuzeeka hapa watoto lazima watawale tu we
utabakia kusema kuwa "nilikuwa nakupiga makofi
zaman" Jaribu sasa huo ubaba wako labda watoto
tu wabaki na ile zana ya kukuogopa na heshima, ila
ata heading yangu haiusiani na familia ngoja niende
nitakako maana inachosa sana japo nitafupisha...

Miaka ya 1950 katika klabu ya Manchester united
kulikuwa na kizazi cha watoto ambao ni hatari
kikosi cha Manchester mpaka mwaka 1957
kulikuwa na wastani wa miaka 21 pia tunakumbuka
sana kile kitu kikosi chao cha "Busby Baby" chini
ya kocha Matt Busby ni Manchester ambayo ilikuwa
tishio huku ikiwa na yule kijana "Big Dun" ambae ni
mchezaji ambae alikuwa na kasi,nguvu na akili ya
kumiliki mpira Man utd walikuwa si timu ya kuomba
kukutana nao maana ulikuwa unapigwa mipira
mwingi ila 1958 kikosi chote kilipotea baada ya ile
ajali ya February nchini Ujerumani Man utd ikapotea
maana wachezaji wao wengi walikuwa...

Ujio wa Fegurson miaka ya 1986 novemba ila
mpaka kufikia mwaka 1992 alitoa vijana sita ambao
ni Ryan Giggs, Beckham, scholes na Neville United
ya miaka ya 1990-2013 imetwaa EPL Mara 13 kwa
hesabu ya haraka tunaweza sema kila baada ya
msimu mmoja walikuwa wanatwaa ubingwa kwa
kipindi cha miaka ya 1992-2013 Enzi za SAF
ilikuwa sio Manchester ya kuangaisha na timu
kama Swansea,Fulham, Hull nk nikikumbuka wakati
msimu wa 1998-99 pale wakina Sheringham na Ole
Gunnars wakifunga magoli dakika za mwisho kabisa
katiaka fainali ya Champion league hiyo ilikuwa
Manchester ya dakika 90 ndio useme umeshinda
kiukweli ilikuwa kila shabiki anajua kuwa wakienda
kucheza basi alama 3 zao Kiukweli kablu ya
Manchester united ilikuwa inaonyesha ule ubaba
wake kwa watoto kwa kutoa kichapo uoasavyo.


Mwanzoni nilisema kuwa ata Baba baadae anakuja
kuzeeka Kiukweli Manchester united sasa hivi
kama ni Baba basi amezeeka maana tangu 2013
kuondoka kwa SAF kumekuwa na matokeo mabovu
haijachukua kombe la ligi kuu la uingereza, Mara ya
mwisho kucheza champion league ni msimu wa
2013-14 ambapo waliishia robo fainali nasema
Baba wa Ukweli HAJITAMBULISHI sasa hivi
mashabiki wa Manchester united tumekuwa
tunaongoza kwa kujitapa kuwa sie ni mabingwa wa
Uefa Mara tatu (3) tunawatambia Chelsea ambao
wametwaa Mara moja huku tukiwaponda Arsenal na
jirani zetu Man City kuwa hawatochukua ilo taji, Sisi
tumechukua Mara nyingi EPL kwahiyo poleni sana
Chelsea kiukweli hizi ni njia za kujifariji tu hakuna
mtu anaependa timu yake iwe na matokeo mabaya
tunakosa kuchukua alama tatu (3) kwa Swansea je
Liverpool au Chelsea kiukwel Man utd mkifungwa
sio mkimbilie mitandao kupost kuwa nyie ndio
mmetwaa Mara nyingi EPL Kiukweli BABA
HAJITAMBULISHI
Mbona wenzenu AC Millan wameshakubali kuwa
kwa sasa ni Baba wa jina tu lakini ule uwezo wa ata
kucheza champion league hana ila nyie
mnajitambulisha kuwa ninyi mababa HATUTAKI
mtuambie ila sisi tunatasema kuwa wewe ni baba
name pia tunautaka ubaba mfanye uwanjani kwa
kutoka na alama maana msimu ndio huo unaelekea
kuisha round ya kwanza na timu ni ya sita kwenye
ligi, Fanyeni vitu ili tuseme kuwa Baba ndio huyu ata
ukicheza na klabu kama Leicester, West
ham,Spurs, walikapa sare tuseme kuwa Spurs
kajitaidi ametoa sare na Baba la Baba Sio mnatoa
sare mnafurahia au mnaogopa kucheza champion
league mnalitaka UEFA ZE COMEDY CUP? Baba
HAJITAMBULISHI ebu Manchester rudini kwenye
mpambano watoto wajue kuwa wanababa.
 
Manchester united mabingwa mara 20 wa EPL.
Sisi ndio baba wa ligi
 
Nimepata shida sana kusoma na kuumaliza uchambuzi wako kwa mujibu wako wewe.

Kwahyo baba akizeeka anageuka kuwa mtoto na mtoto anakua baba au?
 
Nimepata shida sana kusoma na kuumaliza uchambuzi wako kwa mujibu wako wewe.

Kwahyo baba akizeeka anageuka kuwa mtoto na mtoto anakua baba au?
taking example wale vikongwe mkuu wana sifa gani?
 
Back
Top Bottom