marcoveratti
JF-Expert Member
- Sep 21, 2017
- 1,019
- 1,824
8 shots vs Leicester City
9 shots vs Brighton
23 shots vs Tottenham
21 shots vs Burnley
Hakuna bahati hapo, mabadiliko yanatokea ndani ya United.
Kuelekea katika international break takwimu za Manchester United katika michezo minne zinaonekana kushangaza watu kutokana na aina ya mpira wanaoucheza tangu kuanza kwa msimu.
Wanacheza open na mpira wa kushambulia ndio maana imekuwa rahisi wapinzani kuingia kwenye ngome yetu. Unajua sababu gani imekuwa hivyo?
Basi iko hivi, Rui Faria hayupo tena karibu na Jose Mourinho, pembeni ya kocha huyo hivi sasa kuna sura za watu wawili tu huku moja ikionekana kuwa ngeni kwa mashabiki wengi wa United.
Michael Carrick na Kieran McKenna ndio wana mabadiliko ya Manchester United hii ya sasa hasa huyo McKenna ambaye ni mgeni kwenye macho ya watu wengi.
Acha nikusimilie kidogo, wakati Faria anaondoka United kulikuwa na maswali mengi ikiwamo kwa Mourinho ambaye alikaa naye zaidi ya miaka 10 huku kwa kiasi kikubwa akichangia aina ya mpira ambao ulikuwa ukichezwa na kocha huyo.
Moja kwa moja akili ya Mourinho iliekea kwa kocha wa United U-18 ambaye mara nyingi alikuwa akipenda kwenda kuangalia mechi za watoto wakicheza ambao ni wale akina Angel Gomez na Tahit Chong.
Huyo si mwingine bali ni McKenna ambaye mpaka leo moyo wa Mauricio Pochettino umeachwa na jeraha lenye maumivu makali sana baada ya United kumshawishi na kuondoka naye.
Ndio! McKenna ndiye alikuwa msingi wa academy ya Spurs akisifika kwa kuwa kocha mwenye uelewa wa haraka sana lakini pia hata Pochettino kuna kipindi alisema alikuwa anachukua ushauri kutoka kwa kocha huyo aliyekuwa wa vijana pale Spurs.
Kama ulikuwa hujui, yule McKenna ni mtoto wa Spurs kama ilivyo kwa Giggs au kizazi cha 1992 kwa United, mpaka sasa kwenye michezo hii minne binafsi nimemshuhudia Mourinho mpya.
Tazama akili ya McKenna inavyoucheza mpira wa United inawezekana hata usajili wa kuhitaji mabeki ulitoka kwake ili timu iwe salama zaidi pindi wanapokuwa wanashambulia kwa kuwa na ngome kali ya ulinzi.
[source www.mwanaspotiapp.com/mwanaspotiapp]
Sent using Jamii Forums mobile app